Na John Gagarini, Kibaha
                HUKU ikiwa imepita wiki moja ya                  tukio ambalo lilisababisha kifo cha mfanyabiashara wa                  Jijini Dar es Salaam  Mahoro Mlelwa kupigwa risasi na                  majambazi na kufa eneo la Maili Moja wilayani Kibaha                  watu wanaodhaniwa kuwa ni wezi wakiwa na silaha za jadi                  wamevamia maduka na kupora.
        Watu hao walivamia maduka hayo                  baada ya kupiga baruti kwa lengo la kuwatisha watu ili                  waweze kufanikisha wizi huo.
        Akizungumza na waandishi wa                  habari ofisini kwake jana mjini Kibaha kaimu kamanda wa                  Polisi mkoani Pwani, Athuman Mwambalaswa (pichani)                  alisema kuwa tukio hilo lilitokea Septemba 26 mwaka huu                  majira ya saa 2 usiku.
        Kamanda Mwambalaswa alisema                  kuwa mawili yaliyopo eneo la Kwa Mathias wilayani Kibaha                  na kufanikiwa kupora fedha taslimu kiasi cha shilingi                  200,000 pamoja na simu 4 pamoja na vocha za simu zenye                  thamani ya shilingi 200,000.
        "Katika tukio hilo watu hao                  walivamia kwa Godfrey Lunyelele (32) na kumwibia simu                  nne na fedha taslimu kiasi cha shilingi 100,000 na kwa                  Hassan Mkuwili (42) waliiba vocha za simu zenye thamani                  ya shilingi 200,000 na fedha taslimu shilingi 100,000,"                  alisema Kamanda Mwambalaswa.
        Aidha alisema Lunyelele alipata                  ujasiri baada ya kubaini silaha hizo hazina madhara na                  kumpiga kwa tofali kichwani mwizi mmoja kati ya watatu,                  na alipoanguka chini walimkamata na anashikiliwa na                  jeshi hilo kuhusiana na tukio hilo.
        "Mtu tuliyemkamata jina                  linahifadhiwa ili uchunguzi usiharibike na tunaendelea                  kumshikilia ili atupe taarifa za wenzake ambao                  walifanikiwa kukimbia," alisema Kamanda Mwambalaswa.
        Alibainisha kuwa kutokana na                  tukio hilo wamefanya kikao na maofisa wa jeshi hilo na                  kuamua kufanya doria ya nguvu ya miguu pamoja na magari                  ili kuhakikisha wanafanikiwa kudhibiti matukio hayo na                  kuwataka wananchi kutoa taarifa ya watu wanaowadhania                  kuwa ni majambazi.
        Mwisho. 
        .jpg)
0 comments:
Post a Comment