(Pichana Benedict Liwenga,                  Maelezo-Dodoma)
          Na                Benedict Liwenga, MAELEZO-Dodoma.
          MJUMBE                wa Bunge Maalum la Katiba ambaye pia ni Mwenyekiti wa TCD                Mhe. John Cheyo amewataka Watanzania kutodanganywa                kuhusiana na mchakato mzima wa kusaka Katiba Mpya.
           Kauli hiyo imetolewa leo                na Mhe. Cheyo wakati alipokuwa akifanya mahojiano katika                kipindi cha asubuhi cha Jambo kinachorushwa na Televisheni                ya Shirika la Habari Tanzania (TBC).
           Mhe. Cheyo amesema kuwa ni                vema viongozi kuacha kusema uwogo na kuwa waungwana katika                mchakato wa kutafuta Katiba Mpya kwani si vema kuitakia                Tanzania mabaya bali ni kutaka mchakato huo wa Katiba                uendelee kwa amani. Ameongeza kuwa Taifa la                Tanzania linahitaji kuwa Taifa lenye nguvu kwani amani                haiwezu kuwekewa thamani kwa vurugu, hivyo ametaka amani                iliyopo nchini ilindwe na kuepuka kudanganywa na baadhi ya                watu wasiokuwa na nia njema na nchi. Mhe. Cheyo ameshangazwa                kwa kitendo cha viongozi wa UKAWA kutoweka ajenda ya                kurudi ndani ya Bunge hilo wala kuzungumzia kuhusu suala                hilo la kurudi ndani, bali wamekuwa wakitaka wajumbe                wengine walioko ndani watoke kwa kusema kuwa bunge hilo                sio halali.
          "Nawashangaa                UKAWA kwa kutoweka ajenda ya kurudi ndani ya Bunge hili                Maalum la Katiba na badala yake wao wanaweka ajenda ya                kutoka ndani ya bunge hili tena kwa nguvu", alisema Mhe.                Cheyo.
          Aidha,                Mhe. Cheyo amewataka vijana nchini wawe na mshikamano na                kuepuka kudanganywa na viongozi kwa kuambiwa mambo yenye                uwongo huku akisisitiza kuwa Rais aliyeko sasa hivi ana                nia njema ya kuipatia nchi Katiba iliyo bora na yenye                kumfaa kila Mtanzania.
          "Vijana                achene kuvunjika miguu yenu bure, achene kukimbia kimbia                barabarani huku mkilishwa maneno yenye uongo kuhusiana na                mchakato huu wa Katiba, vunjikeni miguu kwa kufanya kazi                kwa bidiii na sio kusikiliza uwongo", alisema Mhe. Cheyo.
          Akizungumzia                kuhusu TCD, Mhe. Cheyo amefafanua kuwa TCD ni Jukwaa la                majadiliano kwa ajili ya maridhiano na mapatano pale                panapokuwa na tofauti kati ya vyama vya siasa.
          "TCD                ni Jukwaa kwa ajili ya kufanya majadiliano na si                vinginevyo, hii ni meza ya maridhiano na nawaambia kuwa                huko mnapokwenda ni kuchepuka, rudini ndani kwenye njia                kuu", alisisitiza Mhe. Cheyo.
          Naye                mjumbe wa Kamati namba Sita ya Bunge Malaam la Katiba Mhe.                Steven Wasira amewaasa Watanzania kwa kusema kuwa, watu                wanaosema kuwa Bunge limenyofoa baadhi ya mambo muhimu                yanayohusu wananchi ni waongo na wenye nia ya kupotosha                Umma wa Tanzania.
          "Kuna                watu wanasema kuwa Bunge Maalum la Katiba limenyofoa                baadhi ya mambo muhimu yanayohusu wananchi huo ni uwongo,                ni mambo gani hayo yaliyonyofolewa? kwasababu kuna mambo                mengi yameongezwa na kuboreshwa katika mapendekezo kwa                ajili ya makundi mbalimbali ndani ya hiyo Rasimu", alisema                Mhe. Wasira.
          Mhe.                Wasira ameongeza kuwa katika Bunge hilo kuna Ibara ya                Rasimu ya Katiba na sio ibara za CCM, amewataka Watanzania                nchini wafanya uchunguzi na kusikiliza kwa kuchambua ili                kupata ukweli wa hayo.
          "Sisi                tuko tayari kuvaana na viopngozi wowote kwani tunataka                Watanzania wote waamini shughuli zifanywazo ndani ya bunge                hili na waepuke kudanganywa", alisema Mhe. Wasira.
        
0 comments:
Post a Comment