Ajali za barabarani duniani hutokea kila uchao, na wahitaji wa damu wanazidi kuongezeka huku idadi ya wachangia damu nayo ikizidi kushuka siku hadi siku na kuleta hatari kwa maisha ya wahitaji.
Kutokana na hali hiyo mji wa Baoji nchini China                  uko kwenye harakati za uhamasishaji uchangiaji wa damu                  kwa mtindo wa kipekee , kampeni ambayo imewekwa ni                  kwamba kama unahitaji kujiunga na chuo,ukitaka kujifunza                  udereva na hata ukitaka kuoa ama kuolewa sharti uchangie                  damu, kampeni ambayo imezua mjadala mkubwa kwenye                  mitandao ya kijamii.
            Sharia hiyo mpya iliyotambulishwa katika jimbo                  la Shaanxi mjini,itaanza kutumika rasmi wiki ijayo                  inawataka askari na wanachuo wa mwaka wa kwanza                  kuchangia damu walau mara moja kwa mwaka .Wananchi wa                  China wanaotaka kuomba leseni za udereva,wanaopokea                  vyeti vya uhitimu wa mafunzo,wanaoajiriwa kwa mara ya                  kwanza, na wale wanaofunga ndoa kwa msajili wa ofizi za                  mji wa Baoji wanapaswa kuchangia damu kwa lazima kama                  mchango wao kwa jamii.
            Taarifa hii ilichapishwa katika mtandao na                  website ya mji huo wa Baoji, lakini kampeni hii                  imekumbwa na changamoto ikiwemo wakaazi wa mji huo                  kuhoji damu hiyo inayotakwa kwa mtindo huo wanahoji                  uchangiaji ukoje na damu hiyo itatumika wapi, badala ya                  kuifikiria Zaidi sharia hiyo mpya.
            Katika jimbo la Pujiang liloko Zheijang wao                  wameichukulia tofauti kampeni hiyo na hivyo wanaongeza                  alama za ziada kwa wanafunzi wa sekondari ambao wazazi                  na walezi wenye utamaduni wa kuchangia damu.
                
            Source:BBC
          
0 comments:
Post a Comment