September 24, mwaka 1976 ni                tarehe muhimu kwenye historia ya siasa na harakati                Tanzania! Ni siku alizaliwa Ndugu Zitto Zuberi Kabwe. Kwa                sasa ni Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini kupitia Chama                cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), nafasi                anayoishikilia tangu mwaka 2005. Zitto, hakuanza harakati                na uongozi baada ya kuingia rasmi kwenye siasa. Katika                kipindi cha mwaka 2002-2003, alishika nafasi ya Katibu                Mkuu wa Baraza la Wanafunzi la Chuo Kikuu cha Dar Es                Salaam. 
            
          Mara baada ya kuhitimu katika                Shahada ya Sanaa katika Uchumi, alikwenda nchini Ujerumani                ambako alikuwa akisomea masuala ya Masoko ya Kimataifa, na                wakati huo huo akisimamia Kurugenzi ya Masuala ya                Kimataifa ya Chadema. Mnamo mwaka 2005, Zitto aliamua                kujiingiza kwenye kinyang'anyiro cha Uchaguzi na                alifanikiwa kutwaa kiti cha Kigoma Kaskazini, nafasi                aliyofainikiwa kuitetea tena katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka                2010. 
          Katika nafasi yake kama Mbunge                alipata pia kutumikia Taifa kama Mjumbe wa Tume ya Rais ya                Kupitia Sekta ya Madini, Kamati ya kuharakisha Mchakato wa                Shirikisho la Kisiasa la Afrika Mashariki kati ya nyingi.                Kwa sasa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za                Serikali. Pia amekuwa akisikika sana katika anga za                Rasilimali hasa akiongelea kwa ukali mapungufu katika                Mikataba ya Uchimbaji wa Madini na Gesi nchini.
           Hivi karibuni Zitto alivuma                sana pale Chama chake kilipomtuhumu kwa Usaliti na                kuanzisha vuguvugu la kumvua uanachama, juhudi ambazo kwa                sasa zimesimama kutokana na pingamizi la kisheria                lililowekwa na upande wake. Pamoja na hayo kumekuwa na                fukuto la fununu za hapa na pale kuwa anaweza kuhama                chama, na kuhamishia harakati zake katika chama                kingine....kipya au kilichopo tangu zamani!
           Mwaka huu 2014 haukuwa mzuri                sana kwani akiwa katikati ya tuhuma za usaliti wa chama,                Zitto alipatwa na Msiba wa Mama Yake kipenzi, na mhimili                wake mkuu wa faraja na hamasa. Zitto hakutueleza sana                kuhusu maisha yake binafsi, ila kama alivyonukuliwa katika                mahojiano na Mkasi, alitumia msemo maarufu toka kwenye                wimbo wa Hamis Mwinjuma (Mwana FA) maarufu kama "Bado Nipo                Nipo", akimaanisha bado hajaoa. Mengi zaidi, endelea                kumsikiliza na kutazama show yetu siku alipoamua kuja                kwenye Kijiwe cha Mkasi kuongea na Wanamkasi!
            Furahia! 
           L•O•V•E
        
0 comments:
Post a Comment