Meza kuu, viongozi wa Chama cha                Mapinduzi Wilaya ya Mbarali na Kata ya Chimala katika                sherehe za kumtambulisha Kamanda wa Vijana (UVCCM) kwenye                matawi ya chama hicho.
                     Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa                CCM, Leonard Kitalima akizungumza jambo kabla ya                kumtambulisha Kamanda wa Vijana wa Kata ya Chimala.
                      Kamanda wa vijana wa UVCCM Kata ya                Chimala, Francis Mtega akifuatilia kwa makini sherehe za                kumtambulisha kwenye matawi.
                     Kamanda wa vijana wa UVCCM Kata ya                Chimala, Francis Mtega akifungua jiwe la wakereketwa la                UWT katika kilabu cha Songambele tawi la Mengele kwenye                sherehe za kumtambulisha kwenye matawi.
                     Kamanda wa vijana wa UVCCM Kata ya                Chimala, Francis Mtega akipandisha bendera katika kijiwe                cha wakereketwa cha Songambele tawi la Mengele  kwenye                sherehe za kumtambulisha kwenye matawi.
                    baadhi ya Wanachama wa Chama cha                  Mapinduzi wakiwa kwenye sherehe za kumtambulisha Kamanda                  wa Vijana kata ya Chimala 
          WANANCHI nchini                wametakiwa kutii amri halali zinazotolewa na jeshi la                Polisi ili kuepuka kujiingiza kwenye vurugu zisizokuwa na                msingi wowote ikiwa ni pamoja na kutii utawala wa sheria                bila shuruti.
          Wito huo                ulitolewa jana na Kamanda wa Umoja wa Chama cha                Mapinduzi(UVCCM), Kata ya Chimala wilayani Mbarali Mkoa wa                Mbeya,Francis Mtega, wakati akitambulishwa kwenye matawi                ya chama hicho.
          Alisema kazi ya                Wanasiasa ni kuwaelekeza wananchi namna ya kufanya kazi                ili kupata maendeleo ili kuinua uchumi wao na sio                kuwahamasisha kufanya maandamano na kukaidi amri halali za                jeshi la polisi hali inayozua vurugu kwenye jamii na                kurudisha maendeleo nyuma.
          Aliongeza kuwa                endapo kila mtu atakuwa akijishughulisha na kazi za                maendeleo hakuna mwanasiasa atakayeweza kumshawishi                kufanya maandamano wakati akijua atapoteza kipato kutoka                kwenye biashara yake anayoifanya.
          Alitolea mfano                kwa umoja wa vijana kwamba ni taasisi kama zingine hivyo                zinapaswa kujiunga kwenye vikundi na kubuni vitega uchumi                mbali mbali ili kuweza kupata fedha kutoka kwenye                Halmashauri ambazo hutenga asilimia 5 ya mapato kila mwaka                kwa ajili ya kusaidia vijana.\
          Mtega                aliwaambia wananchi waliofurika katika mikutano ya                utambulisho kuwa moja ya majukumu yake ni kuhakikisha                Chama kinashinda katika chaguzi zake na kutoa wito kwa                wananchi na wanachama kumuunga mkono ili kuwa na nguvu ya                pamoja.
          Katika                utambulisho huo, Kamanda Mtega pia alizindua jiwe la                wakereketwa wa Umoja wa Wanawake(UWT) eneo la Songambele                na kusimika bendera katika Tawi la Mengele, Kilabu A na                Kilabu B pamoja na tawi la Muala yote ya Kata ya Chimala.
          Mbali na                kufungua matawi hayo pia Kamanda huyo alioyeongozana na                Madiwani wa Kata, Viti maalumu na Mwenyekiti wa Umoja wa                Wazazi wa CCM wilaya ya Mbarali, Leonard Kitalima,                walikabidhi kadi kwa wanachama wapya 170.
          Sambamba na                shughuli hiyo pia viongozi hao walishiriki harambee ya                ujenzi wa choo katika Kilabu kinachoendeshwa na Umoja wa                Wanawake tawi la Mengele kinachogharimu zaidi ya shilingi                Milioni 1.8.
          Aidha katika                harambee hiyo jumla ya shilingi 570,000 zilipatikana,                ahadi shilingi 650,000 na  kufanya                jumla ya fedha zilizopatika kuwa Milioni 1.2 huku nguvu                ikithaminiwa kufikia shilingi laki 5.
          Na Mbeya yetu
          






0 comments:
Post a Comment