Nimeambiwa kuwa kwa sasa kuna watu wa nguvu kibao wanaenda Samunge,Loliondo na kinachowapeleka sio ishu ya Kikombe cha babu tena sasa hivi ni madini ya dhahabu ambayo inasemekana yamegundulika eneo hilo.
Taarifa kutoka
kijijini hapo zinasema kuwa watu wanaongezeka kijijini hapo kwa ajili ya
kujipatia madini hayo yanayosemekana yapo katika mashamba ya watu na maeneo ya
kingo za Mto katika Kijiji cha Mgongo kilichopo jirani na kwa
Babu.
Diwani wa Samunge
Jackson Sandea amesema kwa sasa kuna zaidi ya watu 4,000 na bado wanaongezeka na
kusema kuwa idadi hiyo ya watu inaweza kuwa zaidi ya kikombe cha babu kwa
kipindi kile.
Ingawa eneo rasmi
zaidi bado halijatjwa ila inasemakana mbali na kupatikana kwenye mto huo pia
dhahabu hiyo ianapatikana hata kwenye mashamba ya watu,kwa sasa Kamishna wa
Madini Kanda ya Kaskazini Alex Magayane amesema wanajiandaa kwenda kijijini hapo
baada ya kupokea taarifa za kugundulika kwa dhahabu kwenye eneo la
Samunge.
Imeandikwa na gazeti
la Mwananchi.
0 comments:
Post a Comment