KAMPUNI ya Vodacom Tanzania imetoa msaada kwa Wananchi wa Wilaya ya Kyela kufuatia mafuriko yaliyoikumba Wilaya hiyo hivi karibuni na kutoa athari kubwa kwa wananchi. Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo kwa Mkuu wa Wilaya ya Kyela, Margareth Ester Malenga, Mkuu wa Kitengo cha Maafa(Vodacom Foundation)kutoka Vodacom, Yesaya Mwakifulefule, alisema baada ya kupata taarifa za mafuriko wilayani Kyela Kampuni ilikaa na kujadiliana namna ya kutoa msaada kwa waathirika hao. Alisema baada ya kuchangishana na kupata shilingi Milioni 10, walikubaliana na kitengo cha Msalaba Mwekundu juu ya vitu vinavyohitajika kwa haraka kwa ajili ya kuwapa msaada waathirika na ndipo walipowakabidhi fedha hizo. Alisema Msalaba mwekundu walinunua Magodoro 500, Vyandarua 500 na mablanketi 500 vyote vyente thamani ya shilingi Milioni 10 ambavyo viliwasilishwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Kyela juzi. Aidha Mwakifulefule alitoa wito kwa mashirika mengine kujitolea kwa hali na mali misaada mbali mbali kwa wakazi wa Wilaya ya Kyela kutokana na kuwa bado na mahitaji muhimu. Alisema hali badi ni tete na maeneo mengi yaliyoathirika bado hayajafikiwa hivyo ni vema taasisi zingine zikajitokeza kusaidia wananchi walioathirika na mafurika hayo. Kwa upande waku Mkuu wa Wilaya ya Kyela, Margareth Esther Malenga, akipokea msaada huo kwa niaba ya wananchi alitoa shukrani kwa kampuni ya Vodacom na Chama cha Msalaba mwekundu kwa msaada walioutoa wananchi wake. Alisema Kampuni ya Vodacom inaubia na Serikali lakini ndani yake imekuwa ikiitumikia jamii na wananchi ambao ndiyo wateja wao na watumiaji wa bidhaa zao lakini wanaguswa na kutoa misaada mbali mbali kwa jamii inapokuwa inahitajika. Mwisho.
Na Mbeya yetu |
0 comments:
Post a Comment