Watu wengi waliokutana na picha hiyo wameifananisha suruali hiyo na nguo maarufu kwa akina dada "kipedo" huku wakidai kuwa viatu alivyovaa ni vya kike.
Omary Nyembo a.k.a Ommy Dimpoz amefunguka ya kwake juu ya madai hayo na kusema..
"Viatu sio vya kike kwasababu, ukisema viatu vya kike it means labda umeende ku-shop kwenye duka la vitu vya kike, na viatu vile mi nimenunua South africa, kipindi tumeenda kumsapoti AY kwenye Channel O. nakumbuka tena siku ambayo nimeenda ku-shop nilikuwa na Dulla Spatan, nilinunua kama pea ishirini thelethini, zilikuwa pea nyingi, unajua nsometimes unaweza kuingia kwenye maduka ukakuta kuna sale nini, kwahiyo nilikuta, galafu na vile vilikuwa ni vyepesi havichukui kilos, kwahiyo nikanunua nunua vile vingi, lakini nime-shop kwenye Mr Price nakumbuka, vilikuwa ni simple......"
"sidhani kama watu wameichukuliaje lakini may be labda fashion ndio imenikosti, lakini naona ni viatu vya kawaida na watu wanavaa, hata ukiangalia ma designers nini hata watu wengi wanavaa, kwahiyo kwa kununua mi nimenunua sehem ya vitu vya kiume na hakikua kimoja kusema labda wamekosea wamekiweka sehem tofauti, ni kwamba viko vingi na design tofauti...." amesema Ommy
0 comments:
Post a Comment