May 14, 2014

  • Nizar Khalfan Agoma Kuondoka Yanga

     
     
     
     
    RIPOTI ya aliyekuwa kocha wa Yanga, Hans Pluijm ilipendekeza kiungo Nizar Khalfan atafutiwe timu ya kuichezea kwa mkopo, lakini kiungo huyo amesema "Hapana siondoki nabaki hapahapa nipambane."
    Akizungumza na Mwanaspoti, Nizar alisema alikuwa na mpango wa kutaka kuomba atolewe kwa mkopo kwenda klabu nyingine atakapopata nafasi ya kucheza zaidi lakini amebadili mawazo na kutaka kupigania namba katika timu hiyo.
     
    "Nilikuwa nataka kuondoka kweli baada ya kuomba kuruhusiwa kwenda timu nyingine lakini sitaki tenma hilo nabaki hapahapa Yanga nataka kupigania nafasi yangu," alisema Nizar ambaye amewahi kucheza Canada.
     
    "Kuna mambo mengi nimepanga kuyafanya katika kipindi hiki cha mapumziko, najua bado nina mkataba na Yanga na siwezi kulazimishwa kutolewa kwa mkopo nitabaki hapa niwadhihirishie Wanayanga kwamba bado nina uwezo."
     
  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.