May 15, 2014

  • MAJANGA BASI LAGONGA LORI NA KUUA WATU 10

     
     
     
     
    WATU 10 wamekufa na wengine 10 kujeruhiwa baada ya basi dogo la abiria walilokuwa wakisafiria kugonga lori lililokuwa na kokoto lililoegeshwa kando ya barabara kisha kupinduka katika eneo la Nyamhongholo, jijini Mwanza.
     Akizungumza na waandishi wa habari katika hospitali ya Rufaa ya Bugando, Daktari wa Idara ya Dharura, Dk Regina Mutayangulwa, alisema miili ya abiria hao na majeruhi walipokewa hospitalini hapo juzi usiku.
    Majeruhi waliolazwa katika wodi za upasuaji ni pamoja na wanawake watatu waliolazwa katika wodi namba 9C na wanaume saba waliolazwa katika wodi namba 6Cna 8E na hali zao zinaendelea vizuri.Soma zaidi>>>>>>
  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.