JINA lake halisi ni Leila Salim Rashid, mtangazaji wa kituo cha radio cha PiliPili FM kinachorusha matangazo yake kutoka Mombasa nchini Kenya.
Lakini wasikilizaji wake wengi wanamfahamu zaidi kama Aunty Leyloo au Malkia wa PiliPili. Anaitisha kwenye kwenye miondoko ya taarab. Anaendesha kipindi cha Chachandu za Taarab Jumatatu hadi Ijumaa saa 4 asubuhi hadi 7 mchana akiwa na mwenzake Mamaa Madikodiko. Kwa pamoja wanajiita "Mijike ya Simba".
Wanapatikana pia siku ya Jumapili katika mambo hayo hayo ya taarab kuanzia saa 8 mchana hadi 12 jioni.
Unaweza kuwasikiliza kwa njia ya internet popote pale ulipo kupitia tunein.com, shoutcast.com au kenya moja.com. Uta-enjoy ile mbaya.
Aunty Leyloo ana utajiri wa vipaji, utajiri wa taaluma na utajiri wa majina.
Mtangazaji huyo anayefanya pia kipindi cha Mapishi, ni mwimbaji na hivi karibuni ameachia wimbo wake mpya wa mduara.
Kesho katika Saluti5 tutakufichulia taaluma yake nyingine, vipaji vyake vingine pamoja na kukuwekea wimbo wake huo mpya unakwenda kwa jina la "Uchekechee".
0 comments:
Post a Comment