CHELSEA imeachana na majezi yao ya rangi ya giza katika mechi zao za ugenini na kurejea kwenye enzi za ung'aavu. Wanakwenda na kitu cha njano juu mpaka chini.
Hizi si jezi ngeni kwa Chelsea. Ndio rangi ambayo imetumika zaidi kwenye jezi zao za ugenini kuanzia miaka ya 60.
Lakini pia ndio rangi ambayo imekuwa na nyota njema kwa Chelsea na kupelekea kutwaa mataji kadhaa kwenye miaka ya 60, 70, 80 na miaka ya 2000.
Jezi hizi zinategemewa kuwa kivutia kwa nyota wao wa Kibrazil Oscar, Willian na Ramires ambao rangi njano ni lulu kwao.
0 comments:
Post a Comment