KOCHA mpya wa Manchester United, Louis van Gaal atakabidhiwa kitita kizito cha pauni milioni 200 ili kufanya usajili wa kishindo Old Trafford.
Sambamba na hilo, Van Gaal atakula mshahara wa pauni milioni 6 kwa mwaka.
Unaijua list ya wachezaji anataka kuwasajili? Hebu itupie macho hii:
KEVIN STROOTMAN
Timu: Roma. Bei: £25m, umrii: 24 mechi alizocheza msimu wa 2013-14: 28. Magoli: 6 anatumia guu la kushoto, ana akili sana uwanjani, lakini maumivu ya goti yanamaanisha atakuwa nje ya dimba hadi mwezi Oktoba.
CESC FABREGAS
Timu: Barcelona, bei: £45m, umri: 27, mechi alizocheza msimu wa 2013-14: 55 magoli: 13 yuko sokoni. United haitahangaika nae iwapo kutakuwa na dalili za mizinguo kama ya msimu uliopita.
TONI KROOS
Timu: Bayern Munich, bei: £18m, umri: 24, mechi alizocheza msimu wa 2013-14: 51 magoli: 4. Alionyesha nia ya kujiunga na United chini ya David Moyes, lakini Van Gaal nae anamhitaji mchezaji huyu aliyemvumbua kutoka kikosi cha vijana Bayern Munich.
MATS HUMMELS
Timu: Borussia Dortmund, bei: £20m, umri: 25, mechi alizocheza msimu wa 2013-14: 28 magoli: 2 amekuwa akisumbuliwa na majeraha lakini ni beki mwenye nguvu. Borussia Dortmund itapoteza moja ya wachezaji wake wakubwa.
HOLGER BADSTUBER
Timu: Bayern Munich, bei: £15m, umri: 25, mechi alizocheza msimu wa 2013-14: 0, magoli: 0, anachukuliwa na van Gaal kama beki bora wa kushoto Ujerumani lakini ndio kwanza anatoka kwenye majeruhi.
LUKE SHAW
Timu: Southampton, bei: £27m, umri 18, mechi alizocheza msimu wa 2013-14: 36, magoli: 0. Atajiunga na Manchester United mara tu baada ya mambo ya ndani thamani yake, yatakapo hainishwa.
SEBASTIAN JUNG
Timu: Eintracht Frankfurt, bei: £7m, umri: 23, mechi alizocheza msimu wa 2013-14: 36, magoli: 1. Ni beki bora wa pili wa kulia Ujerumani baada ya Philipp Lahm,
ARJEN ROBBEN
Katika orodha hii yupo pia winga wa Bayern Munich Arjen Robben.
0 comments:
Post a Comment