May 18, 2014

  • JUMUIYA YA WATANZANIA NCHINI KOREA KUSINI WATEMBELEA KITUO CHA SAMSUNG INNOVATION MUSEUM

     
     
     
     
    Tarehe 17 Mei: Jumuiya ya WaTanzania nchini Korea Kusini ilipata fursa ya kutembelea kituo cha Samsung Innovation Museum kujionea teknolojia mbalimbali zinazotengenezwa na kampuni ya Samsung. Kituo hipo kipo kwenye campus kubwa ya kampuni ya Samsung Electronics mjini Suwon.
    Wanajumuiya WaTanzania nchini Korea wakiongozwa na Mwenyekiti wao Bwn. Rayton Kwembe (wa pili kushoto) ambaye pia ni mfanyakazi wa Samsung Electronics Korea wakiingia katika kituo cha Samsung Innovation Museum.
    Jumuiya ya WaTanzania wakifuatilia kwa umakini maelezo ya historia ya teknolojia mbalimbali zilizosaidia kurahisisha maisha.
    Wanajumuiya wakifuatilia filamu inayoonyesha jinsi bidhaa mbalimbali za Samsung zinavyobuniwa kulingana na mahitaji ya binadamu.
    Wanajumuiya wakipozi kwa picha nje ya kituo cha Samsung Innovation Museum baada ya kumaliza ziara. Hakika ilikuwa ni ziara iliyofungua macho.
    Mandhari ya campus kubwa ya Samsung Electronics mjini Suwon ambayo ndio kitovu cha mafanikio ya Samsung. Campus hiyo ina jumla ya wafanyakazi 40,000 wanaofanya kazi kazi idara za masoko na reseach.
  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.