May 19, 2014

  • Fahamu Sifa za Mwanamke wa Kuoa (Wife Material)

    Wanaume wengi wanapofikia hatua ya kuoa si kwamba wanakurupuka tu na kuoa mwanamke yeyote mwenye sura nzuri, bali huchukua muda wao mwingi kuchunguza mambo mengi juu ya wake ambao wanadhani kwamba wanaweza kuwa pamoja kwa kipindi chote cha maisha.
    Wanawake wengi wanajisahau na kudhani kwamba kitu kinachoweza kuwafanya wakapata wachumba ni uzuri hivyo kupoteza muda wao kujichubua na kujiremba ili wawavutie wanaume bila kujua kwamba kuolewa ni zaidi ya uzuri.
    Hali sasa hivi imebadilika ni tofauti na kipindi cha nyuma ambapo ukiwa na sura nzuri na umbo la kuvutia basi una asilimia 100 za kuolewa.
    Utafiti ambao nimeufanya unaonesha kwamba zaidi ya uzuri wa tabia na umbo, kuna kuna sifa nyingine za msingi ambazo mwanamke anatakiwa kuwa nazo ili aweze kuwa katika mazingira mazuri ya kupata mchumba wa kumuoa kiasi kwamba asipokuwa nazo ataishia kuchezewa tu lakini haitatokea mtu kumtamkia kwamba anataka kumuoa.
    • 1. MWEYE MAPENZI YA KWELI
    • 2.MWENYE TABIA NZURI
    • 3. MWENYE UCHU NA MAENDELEO
    • 4. ASIYEPENDA MAKUU
    • 5. MVUMILIVU
    Mwanamke ukiwa na sifa hizo tano hapo juu unauwakika wa 100% kuolewa.
    Nawasilisha!
  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.