Uongozi wa
Kampuni ya Proin Promotions Limited na Timu nzima ya Kampuni ya Proin Promotions
Limited ambao ni Waandaaji na waendeshaji wa Shindano la Tanzania Movie Talents
tunapenda kutoa pole zetu za dhati kwa Wazazi wa Marehemu Adam P.Kuambia, Ndugu
wa Marehemu , Jamaa, Marafiki kwa ujumla na Rais wa Klabu ya Bongo Movie, Ndugu
Steve Nyerere kwa kuondokewa na Mmoja kati ya Wasanii Mahiri kabisa katika
tasnia hii ya filamu nchini vilevile tunatoa Pole zetu kwa Wasanii wa sanaa ya
Maigizo Tanzania na Klabu ya Bongo Movie kwa kuondokewa na Msanii mwenzao Adam P
Kuambiana.
Kutokana na
Msiba huo wa Marehemu Adam Philip Kuambiana, Uongozi wa Kampuni ya Proin
Promotions Limited ambao ni waandaaji na waendeshaji wa Mashindano ya Tanzania
Movie Talents unapenda kutangaza kusitisha Zoezi la Usaili wa Shindano hilo
lililokuwa linaendelea Mkoani Arusha kwa siku moja kwaajili ya Kuungana na
Watanzania katika Msiba huu Mkubwa ulioikumba Tasnia ya Filamu Nchini Katika
kuomboleza na Kushiriki katika Mazishi ya Marehemu Adam Philip Kuambiana
yanayotarajiwa kufanyika kesho Jumanne tarehe 20 Mei 2014 katika Makaburi ya
Kinondoni.
Kutoka Kwenye
timu ya Tanzania Movie Talents iliyopo Mkoani Arusha, Timu hiyo itawakilishwa na
Mmoja wa Majaji katika Shindano la Tanzania Movie Talents, Ndg Single Mtambalike
ambae anatarajia kusafiri kesho kwa Ndege kutoka Mkoani Arusha kwaajili ya
Kuungana na Watanzania wote na wasanii wengine katika msiba na mazishi ya
Marehemu Adam Philip Kuambiana. Vilevile Ndg Single Mtambalike ataungana na
Wafanyakazi wa Proin Promotions Limited waliopo jijini Dar Es Salaam katika
Msiba huo.
Timu nzima ya
Tanzania Movie Talents iliyopo Mkoani Arusha tunapenda kutoa Pole zetu za Dhati
kwa wafiwa wote na watanzania wote tulioguswa na msiba huu wa Msanii wa Filamu
Nchini Adam Kuambiana.
Shindano la
Tanzania Movie Talents litaendelea kama kawaida siku ya Jumatano asubuhi kama
ratiba ilivyopangwa.
Tunamuomba
Mwenyezi Mungu ailaze Roho ya Marehemu Mahala Pema Peponi –
Amina
Bwana ametoa
na Bwana Ametwaa Jina la Bwana lihimidiwe
Imetolewa
na
Josephat
Lukaza
Afisa
Mahusiano – Tanzania Movie Talents
Proin
Promotions Limited
0 comments:
Post a Comment