May 18, 2014

  • Hapo Safi Patamu: Jumuiya ya Wazazi/CCM Yamfukuza Mmoja na Kuwasimamisha Wengine Wawili!!

     
     
     
     
     
     
    - Toka juzi nipo Dodoma kushiriki kikao cha Baraza Kuu la Wazazi/CCM Taifa jana usiku tumemaliza vikao vyetu na kumfukuza aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wazazi/CCM Taifa Mh. Dadi ambaye bado alikuwa ni Mjumbe wa Baraza hili na pia Mjumbe wa Kamati ya Uekelezaji ya Baraza hili. Pia tumemsimamisha uongozi wa aina yoyote ndani ya Jumuiya yetu Makamu wa Mwenyekiti wa Taifa Mh. Dogo na pia tumemsimamisha Mjumbe wa Baraza hili Mkoa wa Mara Mh. Jeremiah Wambura kwa kukiuka Kanuni za Jumuiya.


    - Hatma ya Mh. Dogo inaenda mikononi mwa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, na hatma ya Mh. Wambura inarudi mikononi mwa Kamati ya Utekelezaji ya Wazazi kwa uamuzi wa mwisho kama afukuzwe kabisa au apewe adhabu nyingine na kusamehewa.

    - Waheshimiwa Dogo na Dadi, wamaetuhumiwa na kanuni za Jumuiya ya Wazazi/CCM Taifa kwa kuiingiza Jumuiya kwenye hasara kubwa sana kwa kujiunga na Family Bank ambayo uchunguzi wa Jumuiya umeonyesha ni benki ambayo haipo, wakafikia mpaka kumualika Rais wa Jamhuri kufungua Benki hiyo ambayo haikuwepo ila ulikuwa ni ujanja ujanja tu na mpaka uongozi wetu mpya ulishika madaraka tumekuta Jumuiya sasa inadaiwa jumla ya Shillingi Millioni 9.8 ambazo walizikusanya toka kwa wananchi kwa uongo wa kuwauzia hisa huku wakijua bayana kwamba benki hiyo haipo, tunategemea baada ya yote wahusika wote kufikishwa mahakamani baada ya utaratibu wote wa kisheria kufuatwa.

    - KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI!!
  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.