DAVID Luiz wa Chelsea yuko njiani kutua Paris St Germain ndani ya masaa 48 yajayo katika usajili unaotegemewa kuwagharimu mabingwa hao wa Ufaransa kiasi kinachokaribia pauni milioni 50.
Ingawa makubaliano halisi ya timu hizo mbili hayako wazi, lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 anatarajiwa kuwa beki ghali duniani akivunja rekodi ya Mbrazil mwenzake Thiago Silva na Marquinhos walionunuliwa na PSG kwa bei mbaya.
Mara makubaliano yatakapofikiwa, PSG wataomba idhini ya kocha wa Brazil Luiz Felipe Scolari ya kumruhusu mchezaji huyo kuondoka kwenye kambi ya Kombe la Dunia kwenye kufanya vipimo vya afya.
PSG wanaamini kuwa wanamnasa beki mwenye soka la aina yake ambapo usiku uliopita walioneka kuwa tayari kulipa kitita wanachokihitaji Chelsea.
0 comments:
Post a Comment