September 01, 2014

  • Balozi Mdogo wa Tanzania- Dubai akutana na Mtendaji Mkuu wa Dubai Chamber of Commerce and Industry


    Balozi Mdogo wa Tanzania- Dubai akutana na Mtendaji Mkuu wa Dubai Chamber of Commerce and Industry
    Mhe. Omar Mjenga, amekutana na Mhe. Hamad Buamim, Rais na Mtendaji Mkuu wa Dubai Chamber of Commerce and Industry na kufanya naye mazungumzo.

    Katika mazungumzo, wamejadiliana uwezekano wa kuwa na ziara ya kibiashara kwenda Tanzania, kwa makampuni na viwanda vilivyopo Dubai, ili kukutana na wafanyabiashara na wamiliki wa viwanda Tanzania, ili kujionea na kuibua fursa za uwekezaji. Wamekubaliana ziara hiyo ifanyike mwanzoni mwa mwaka kesho na hivyo basi kuanza maandalizi mapema.

    Mwezi Novemba, kutakuwa na ziara ya kibiashara ya makampuni kutoka Falme ya Ajman.

    Aidha, wamezungumzia kuhusu mkutano wa Africa Global Business Forum utakaofanyika tarehe 1-2 Oktoba 2014 hapa Dubai. Mtukufu Sheikh Mohammed bin Rashid al Maktoum amemwalika Rais Kikwete kuhudhuria pamoja na marais wengine wa Mali, Ghana, Uganda, Mozambique, Ethiopia, Senegal, Burkina Faso, Sudan na Ivory Coast.

    Mkutano huu hufanyika kila mwaka ambao huzungumzia njia muafaka ya ushirikiano kati ya Serikali ya Dubai na UAE kwa ujumla na nchi za Afrika.


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.