
Jiwe kubwa Likiwa limeanguka toka mlimani na kuziba Barabara ya Vuga Kutoka Mombo kuelekea korogwe na Lushoto


Kwa juu ni mlima ambapo jiwe hilo liling'oka na kudondoka hatimaye kuziba barabara hiyo kwa takribani masaa sita

Abiria na madereva wakiwa wamekaa wakisubili mamlaka zinazohusikka wafike ili kutoa msaada wapate kuendelea na safari.

Vyombo vya dola wakiwa wamefika eneo la tukio tayari kuweza kulisogeza jiwe hilo ili abiria na watumiaji wa barabara ya vuga kuendelea na shughuli zao

Hayo ni baadhi ya mawe ambayo yanaonekana kwa juu ya barabara ya vuga inayounganisha kutoka mombo kuelekea lushoto.
Hali ya usafiri kutoka mombo-korogwe kuelekea wilaya ya Lushoto mkoani tanga ilikuwa tete baada ya jiwe kubwa kuangua barabarani katika eneo la vuga road.Jiwe hilo lilisababisha wasafiri wa barabara hiyo kukwama kwa takribani masaa 6 bila magari kupita.Lakini hatimaye baadae vyombo vya usalama wakishirikiana na wanainchi waliweza kulitoa na hatimaye usafiri wa njia hiyo kurejea katika hali yake ya kawaida.
0 comments:
Post a Comment