Kuna msemo usemao kuwa 'kinyozi ndiye fundi pekee mwaminifu' kwa kuwa hana tabia ya kufanya kazi nusu na kumwambia mteja 'njoo kesho'.
Pia, kionyozi amepewa sifa ya kufanya kazi moja kwa wakati mmoja, huku akisimamiwa na mteja wake ambaye analazimika kuwapo muda wote wakati wa kupata huduma.Hata hivyo, pamoja na sifa zote hizo, kinyozi anakumbana na changamoto mbalimbali ambazo nyingine zipo nje ya uwezo wake, likiwapo suala la watu kwenda kwa kinyozi kuiba nywele za wateja.
Katika hali ya kawaida mtu huenda saluni kunyoa nywele na kuziacha hapo bila kufikiria kuwa nywele hizo zinapelekwa wapi. Uchunguzi uliofanywa na gazeti la mwananchi jijini Dar es Salaam umebaini kitu cha kushangaza kuhusu hofu waliyonayo watu juu ya nywele zao.
Wapo baadhi ya watu ambao huenda saluni kunyoa nywele huku wakitoa masharti magumu kwa vinyozi. Wateja hao hutaka kujua nywele zao zitapelekwa wapi baada ya kunyolewa, ni nani atakayekuja kuzichukua huku wengine wakitaka kuwa wa kwanza au mwisho kunyolewa.
0 comments:
Post a Comment