Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Exim Tanzania, Bw. Yogesh Manek akishiriki zoezi la Ice Bucket Challenge kuunga mkono kampeni dhidi ya ugonjwa wa fistula nchini Tanzania, baada ya kuteuliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania Bw, Sunil Colaso. Tukio hilo lilifanyika katika ofisi za makao makuu ya benki hiyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Exim Tanzania, Bw. Yogesh Manek akizungumza na waandishi kabla kushiriki zoezi la Ice Bucket Challenge kuunga mkono kampeni dhidi ya ugonjwa wa fistula nchini Tanzania, baada ya kuteuliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania Bw, Sunil Colaso. Tukio hilo lilifanyika katika ofisi za makao makuu ya benki hiyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
======== ====== =========
Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Exim Tanzania, Bw. Yogesh Manek ameshiriki katika Ice Bucket Challenge, kuunga mkono kampeni dhidi ya ugonjwa wa fistula nchini Tanzania, baada ya kuteuliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania Bw, Sunil Colaso.
Kabla ya kumwagiwa maji yenye barafu Bw. Manek aliwateua, Ali Mafuruki Mwenyekiti na Afisa Mtendaji Mkuu wa Infotech Investment Group, Shabir Abji, Mwenyekiti wa Hotel ya New Africa na Veena Jog, Mkurugenzi Mtendaji wa Advent Constructions Ltd kushiriki katika zoezi hilo ikiwa ni jitihada za kuwaokoa wanawake wakitanzania wenye tatizo la ugonjwa huo wa fistula.
Akizungumza kabla ya kushiriki, Jumapili, Bw. Yogesh Manek alisema amehamasika kukubali shindano hilo kutokana na idadi kubwa ya maisha inayopotea na ulemavu unaosababishwa na ugonjwa huo: pamoja na zoezi hilo kunakshiwa na mpango wa utunzanji mazingira wa benki hiyo ujulikanao kama 'Exim Go Green' Maji kwa matumizi mazuri.
"Namshukuru Bw. Sunil Colaso, Mkurugenzi wa Airtel Tanzania, kwa kunichagua kufanya zoezi hili ambalo nimelipokea kwa heshima kubwa sababu nafahamu urishiriki wangu utaukoa maisha ya walio wengi na kusaidia Tanzania kuwa huru dhidi ya fistula. Kwa mujibu wa takwimu zilizopo zaidi ya wanawake 8000 ufariki kutokana na fistula, 160,000 upata ulemavu na zaidi ya watoto 40,000 wa chini ya mwaka mmoja ufariki kutokana na ugonjwa huu unaotibika," alisema.
Alibainisha kuwa Benki ya Exim, imekuwa ni katika mstari wa mbele kuunga mkono shughuli mbali mbali zenye manufaa kwa wanawake, ndiyo maana kampeni ya fistula imekuja kwa wakati muafaka.
"Benki ya Exim imekuwa ikiunga mkono miradi mbali mbali ya kimaendeleo ya kijamii, hususani katika sekta za afya, mazingira na elimu.
"Hii imethibitishwa na baadhi ya shughuli za kijamii tulizofanya hivi karibuni, ikiwa ni pamoja na kuchangia magodoro katika hospitali ya Mwananyamala, kuijengea shule ya msingi Kilakala vyoo na kushiriki kikamirifu katika shughuli za usafi wa mazingira nchi nzima, ili kuwa na mazingira safi.
"Na leo hii, ninashiriki katika Ice Bucket Challenge kuonyesha jitihada zetu kama benki katika kuendelea kuunga mkono shughuli hizo," alisema Bw. Manek. Alisema kuwa wafanyakazi wote wa Benki ya Exim wameunga mkono zoezi hili la Ice Bucket Challenge ambalo limeanzishwa kwa lengo zuri.
"Tunafuraha kubwa na kiwango cha huruma, ukarimu na hisia zilizoonyeshwa na wafanyakazi wote, wao pia wakishiriki katika zoezi hili muhimu kikamirifu," alisema Bw Manek.
Bw. Manek alibainisha pia, zoezi hilo pia limelenga katika kukuza ushiriki wa wafanyakazi na watu wengine katika shughuli za kijamii ambazo benki imekuwa ikianzisha mara kwa mara ikiwa na lengo la kusaidia kukuza sekta mbali mbali za kiuchumi na kijamii nchini.
Benki ya Exim ni moja kati ya benki kubwa nchini kwa upande wa mali zake za jumla, na kuwa na matawi 32 nchi nzima ikisambaa katika uchumi wa nchi tatu Afrika.
0 comments:
Post a Comment