Baadhi ya silaha zilizokamatwa na jeshi la polisi.
Baadhi ya wanahabari wakimsikiliza Kova.
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia mtu mmoja anayefahamika kwa jina la Gunner Meena (40) mkazi wa Kinyerezi, Segerea, Dar es Salaam, kwa tuhuma za kujifanya mtumishi wa Idara ya Usalama wa Taifa .
Tukio la mwisho lililomfanya akamatwe ni pale alipomtishia mfanyabiashara mwenye asili ya Kisomali aitwaye Abdi Dalmar, ili ampe Tshs 25,000,000/= ama sivyo angechukua hatua chini ya Sheria ya Usalama wa Taifa.
Aidha jeshi hilo katika kuendesha oparesheni zake za kutokomeza ujambazi wa kutumia silaha limefanikiwa kukamata bastola nne na shot-gun moja wiki hii.
0 comments:
Post a Comment