Mwanamke mmoja                    mwenye umri wa miaka 19 amekutwa amening'inizwa juu ya                    mti katika kijiji kimoja Kaskazini mwa India, likiwa                    ni tukio la tatu kutokea ndani ya wiki moja katika                    Jimbo la Uttar Pradesh.Mwili wa mwanamke                huyo umekutwa katika eneo la Moradabad ambapo familia yake                imewaambia polisi kuwa alibakwa huku uchunguzi wa                madaktari ukiendelea kufanyika.Mwanamke mwingine alikutwa                amening'inizwa juu ya mti katika Jimbo la Uttar Pradesh                siku ya Jumatano.Mwezi uliopita mabinti wawili wadogo                walibakwa na kundi la watu katika mazingira kama hayo na                kuibua maandamano ya hisia kali nchini India.
            Siku                    ya Jumatano, mwanamke mwenye umri wa miaka 44 nae                    alikutwa amening'inizwa juu ya mti katika eneo la                    Bahraich.
                Polisi                    wamesema kuwa alikuwa akipatiwa vitisho na wanakijiji                    kwa kuuza pombe katika eneo hilo na familia yake                    ilifungulia kesi watu watano kuhusiana na kifo hicho.
              
 
 
 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment