Mzee Yusuph (Kulia) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa utambulisho wa filamu yake ya Kwanza iitwayo NITADUMU NAE ambapo filamu hiyo imeingia sokoni leo Jumatatu na inasambazwa na Kampuni ya Proin Promotions Limited, Kushoto ni Meneja Masoko wa Kampun ya Proin Promotions Limited, Evans Stephen.
Mzee Yusuph akibadilishana Mkataba na Mwanasheria wa Kampuni ya Proin Promotions Limited Halima Mara baada ya Kumaliza kutiliana saini katika Mikataba. Na Josephat Lukaza - Proin Promotions Limited
Hatimaye Mzee Yusuph atambulisha rasmi ujio wake katika Tasnia ya Filamu leo mara baada ya kuitambulisha filamu yake mpya na ya Kwanza iitwayo NITADUMU NAE ambapo filamu hiyo ni moja ya filamu ambazo zimetoka katika nyimbo zake.
Akiongea na Waandishi wa Habari Mzee Yusuph alisema "Filamu hii nimeitengeneza muda mrefu sana na imetoka katika nyimbo zangu lakini nilishindwa kuisambaza kutokana na kukosa Msambazaji ambaye anaweza kukubaliana na vigezo vyangu lakini Kwa bahati nzuri Proin Promotions imeweza kuwa na vigezo ambavyo mimi nimekubaliana navyo na nimeridhika navyo ndio maana nimeona wanaweza kusambaza filamu yangu"
Na Pia ameelezea sababu kubwa ya yeye kuamua kufanya kazi na Proin Promotions ni kwamba "Kampuni ya Proin Promotions hainunui hakimiliki za wasanii ndio maana nimeona nifanye nao kazi"
Vilevile Filamu ya Mzee Yusuph ishaingia sokoni leo na inasambazwa na Kampuni mahiri ya Proin Promotions Limited ambapo filamu hiyo inapatikana Nchi nzima kuanzia leo.
Mbali na hiyo pia Mzee Yusuph amesema kuwa sasa anabadili nyimbo zake kwenda kwenye filamu kwasababu nyimbo zake zote zina uwezo mkubwa wakuwa filamu ndio maana kwa kuanza ameanza na Nyimbo yake ya Nitadumu Nae.
0 comments:
Post a Comment