August 25, 2014

  • WANANDOA WAKRISTO WAINGIA MATATANI KWA KUKATAA WASAGAJI KUTUMIA BUSTANI YAO



    WANANDOA WAKRISTO WAINGIA MATATANI KWA KUKATAA WASAGAJI KUTUMIA BUSTANI YAO
    Uwanja unaomilikiwa na wanandoa wakristo waliopinga ndoa ya jinsia moja kufungwa hapo.©LibertyRidgeFarmNy.com
    Mahakama moja jijini New York nchini Marekani imewatoza faini mke na mume kwa kosa la kuwakatalia wapenzi wa jinsia moja (wasagaji) kutumia bustani yao kwaajili ya kusherehekea harusi yao kwa madai ni kinyume na imani na matakwa yao.

    Cynthia na mumewe Robert Gifford hukodisha uwanja wao wenye ukubwa wa ekari 100 kwa ajili ya matukio mbalimbali yakiwemo harusi, matamasha, sherehe mbalimbali na matukio mengine na kwamba wamesema uwanja huo binafsi ambao pia kuna nyumba yao ya familia wanayohaki ya kuruhusu ama kukataa maombi ya mtu anayetaka kuutumia jambo ambalo mahakama limepinga.

    Kwa mujibu wa jaji Migdalia Peres katika hukumu yake amesema kitendo kilichofanywa na wanandoa hao ni kinyume cha haki za binadamu na kwamba pamoja na kutakiwa kulipa faini ya dola za kimarekani 13,000 sawa na milioni 21, 599, 500 lakini pia wameitaka familia hiyo kubandika matangazo katika bustani hiyo ya kuonyesha wanaruhusu watu wa jinsia zote kutumia bustani yao, sambamba na kuwaelemisha wafanyakazi wao katika bustani hiyo juu ya kuheshimu watu wa aina zote.

    Melissa Erwin pamoja na Jennifer McCarthy walionyesha nia yao ya kutaka kutumia bustani hiyo kwa harusi yao mwezi September mwaka 2012 lakini wanandoa hao walikataa wasagaji hao kufunga ndoa yao katika bustani hiyo ingawa walikuwa tayari kuwaruhusu kutumia kwaajili ya sherehe mara baada ya kufunga ndoa yao jambo ambalo watu hao walilipinga na kufungua kesi ya kudai kitendo cha kuzuiwa kufunga ndoa katika bustani hiyo kilikuwa kimevuruga akili yao hasa kwakuwa walihitaki kutafuta mahali pengine pa kufanya tukio hilo.

    Habari za zaidi na kwa undani BONYEZA HAPA



  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.