September 04, 2014

  • MMOJA NA WENZAKE WAWILI MBARONI KWA KUKUTWA NA PEMBE ZA NDOVU MKOANI DODOMA


    MMOJA NA WENZAKE WAWILI MBARONI KWA KUKUTWA NA PEMBE ZA NDOVU MKOANI DODOMA
    Na. Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma.

    Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linamshikilia mtu mmoja aliyefahamika kw ajina la DOUGLAS S/O MNYEKE, Miaka 46, Mkaguru Mukulima na Mkazi wa kijiji cha Silwa Kata ya Pandambili, Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma akiwa na pembe za ndovu vipande vitatu vyenye uzito wa jumla ya kilo 12 na gramu 30 vyenye thamani ya Tshs. 11, 162, 250/= vikiwa nyumbani kwake.

    Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME – SACP amesema tukio hili limetokea tarehe 30/08/2014 majira ya 15:02hrs katika kijiji cha Silwa Kata ya Pandambili, Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma.

    Kamanda MISIME amesema baada ya mtuhumiwa huyo kuhojiwa alikiri kuwa na mzigo ndani  ya nyumba yake  wenye vipande vinne vya pembe za ndovu vikiwa kwenye mfuko wa salfeti maarufu kama kiroba cheupe na kueleza kuwa aliletewa na watu wawili ambao ni NORBERT S/O KAHWIL, Miaka 32, Mbena, Mkulima wa Ngomai Wilaya ya Kongwa na BONIFACE S/O MASINGISA, Miaka 30, Mkaguru, Mkazi wa Silwa Kata ya Pandambili Wilaya ya Kongwa.

    Aidha Kamamnda MISIME amesema watuhumiwa wote watatu walikamatwa na wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma kwa uchunguzi zaidi na pembe hizo zimehifadhiwa kama kielelezo pia watafikishwa mahakamani mara baada ya taratibu kukamilika.


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.