June 17, 2014

  • Watoto Pacha Kufanyiwa Operesheni Nyingine Kuwekewa Njia ya Mkojo ya Kawaida




    Watoto Pacha Kufanyiwa Operesheni Nyingine Kuwekewa Njia ya Mkojo ya Kawaida
    Watoto pacha waliotenganishwa, Eliud na Elikana watafanyiwa upasuaji mwingine ili kuwatengenezea njia ya mkojo ya kudumu.
    Pacha hao walizaliwa wakiwa na njia moja ya haja kubwa na ndogo, hali iliyowapa wakati mgumu madaktari wakati wa operesheni ya kuwatenganisha.
    Akizungumzia hali ya Eliud baada ya kufanyiwa upasuaji wa kurejesha utumbo wake ambao ulijitokeza, Mkuu wa Kitengo cha Upasuaji wa Watoto, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dk Zaituni Bokhary alisema hali yake inazidi kuimarika.
    Alisema pia kuwa, wiki hii watamfanyia upasuaji Elikana ili kuirudisha ndani sehemu ndogo ya utumbo wake ambayo nayo ilikuwa nje. Baada ya kukamilika kwa upasuaji huo, tatizo la njia ya haja kubwa itakuwa imetatuliwa kama ilivyo kwa mwenzake.

    Dk Bokhari alisema baada ya kupona, watoto hao watafanyiwa upasuaji mwingine ili kurekebisha njia zao za mkojo na kuzifanya za kudumu. Alisema kwa sasa wanatumia njia za haja ndogo walizotengenezewa kwa ajili ya kutumika kwa muda mfupi.

    Alisema kabla ya upasuaji wa kuwatenganisha, pacha hao walikuwa na njia moja ya mkojo pamoja na uume mmoja. Hata hivyo, njia ya mkojo ilikuwa chini ya korodani badala ya kupita katika uume.

    "Baada ya miezi mitatu, watafanyiwa upasuaji mwingine ili kuziba tundu la njia ya mkojo na kuwatengenezea njia nyingine ya kawaida," alisema na kuongeza kuwa tatizo hilo linawakumba hata watoto wengine nchini.

    Baba wa watoto hao, Eric Mwakyusa alisema Eliud anaonekana mwenye furaha baada ya operesheni hiyo tofauti na alivyokuwa awali utumbo wake ulipokuwa umejitokeza nje.

    Pacha hao walipelekwa India mwaka jana kwa ajili ya upasuaji mkubwa wa kuwatenganisha ambao ulifanikiwa. Hata hivyo, sehemu ya utumbo mpana wa Eliud ilijitokeza nje kabla ya kufanyiwa upasuaji mdogo hivi karibun


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.