June 20, 2014

  • WANAFUNZI DAR ES SALAAM WAVUTIWA NA SHUGHULI ZA NISHATI NA MADINI


    WANAFUNZI DAR ES SALAAM WAVUTIWA NA SHUGHULI ZA NISHATI NA MADINI
    6Mhandisi wa Nishati kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Robert Dule, akiwaeleza wanafunzi kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu nishati wakati wanafunzi hao walipotembelea banda la Wizara.7Watumishi wa Wizara ya Nishati na Madini na baadhi ya Watumishi wa Taasisi zilizo chini yake wakiwa katika picha ya pamoja katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.

    ………………………………………………………………..

    Na Asteria Muhozya, Dar es Salaam
    Baadhi ya Wanafunzi kutoka baadhi ya Shule za Sekondari mbalimbali Jijini Dar es Salaam wametembelea banda la Wizara ya Nishati na Madini na Taasisi zilizo chini yake kutaka kufahamu shughuli mbalimbali zinazofanywa na zinazofanyika. 
    Wakati wanafunzi hao walipotembelea Wizara na Taasisi zake, wameoneshwa kuvutiwa na kutaka kufahamu kuhusu namna shughuli za uchimbaji madini nchini zinavyofanyika, kutaka kufahamu aina za madini yenye thamani kubwa na  madini yenye uzito mkubwa.
    Vilevile, wanafunzi hao wametaka kuelimishwa kuhusu shughuli za utafiti na uchimbaji wa gesi zinazofanyika nchini ikiwa ni pamoja na kutaka kufahamu vyuo mbalimbali vinavyotoa mafunzo kuhusu masuala ya gesi, mafuta na madini.
    Aidha, wengi wao walipenda kuona madini ghafi ya Tanzanite yanayopatikana nchini ikiwa ni pamoja na kufahamu aina zote za madini yaliyopo chini. Wanafunzi hao wamepata nafasi ya kupata majibu kuhusu masuala mbalimbali waliyouliza kutoka kwa waatalamu mbalimbali wa Wizara na Taasisi waliopo katika maonesho hayo.


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.