BAADA ya kuingoza England kwenye michuano ya kombe la dunia na kufanya vibaya kupindukia, kocha Roy Hodgson angetimuliwa kama angekuwa ni kocha wa kigeni.
Hayo yamesemwa na kocha wa zamani wa England Sven-Goran Eriksson (pichani juu) ambaye aliikochi England mwaka 2001 hadi 2006.
Lakini licha kufanya vibaya kuliko mara zote ambazo England imeshiriki World Cup, kibarua cha Roy Hodgson kipo kwenye mikono salama.
Eriksson ameliambia Sunday Telegraph kuwa kama angekuwa yeye ndiye aliyekwenda na timu ya England huko Brazil na kupata matokeo hayo, angetimuliwa mara moja.
Hata hivyo Eriksson amesema Roy Hodgson ni kocha bora na England wanastahili kumbakiza.
0 comments:
Post a Comment