TETESI barani Ulaya zinasema kuwa kiungo wa Bayern Munich anayewaniwa na Manchester United, Toni Kroos yuko kwenye nafasi kubwa ya kujiunga na mabingwa wa Ulaya, Real Madrid.
Gazeti linaloheshimika nchini Ujerumani, Bild, limeripoti kuwa mazungumzo kati ya Bayern Munich na Real Madrid yapo katika hatua nzuri juu ya nyota huyo wa Ujerumani.
Inaaminika Real Madrid wamempa Kroos ofa ya mshahara wa pauni milioni 4 kwa mwaka na sasa miamba hiyo ya Hispania inasubiri jibu kutoka kwa wakala wa mchezaji huyo, Volker Struth.
Habari hizi zitakuwa ni pigo kubwa kwa Manchester United ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakivutiwa na kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24.
Kuingia kwa Real Madrid kwenye dili la Kroos limekuja siku chache baada ya gazeti la El Confidencial kuripoti kwamba Louis van Gaal alimpigia simu Kroos na kumshawishi ajiunge na Manchester United.
Kiungo wa Borussia Dortmund ambaye nae pia alikuwa anatajwa kuwaniwa na Manchester United, Marco Reus, amehusishwa na safari ya kujiunga na Barcelona wakati Cesc Fabregas aliyeumiza vichwa vya United tangu msimu uliopita, anakaribia kumalizana na Chelsea.
0 comments:
Post a Comment