June 10, 2014

  • M-PESA YAENDELEA KURAHISISHA HUDUMA KWA WATANZANIA




    M-PESA YAENDELEA KURAHISISHA HUDUMA KWA WATANZANIA
    Dar es Salaam,Tanzania Juni 10, 2014 , Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2008, huduma ya M pesa imendelea kuwa huduma yenye mafanikio zaidi katika utoaji wa huduma za kifedha huku ikiwanufaisha watanzania ambao wanauwezo wa kutuma na kupokea pesa kupitia mawakala zaidi ya 70,000, walioenea nchini kote.

    Akizungumzia mafanikio ya huduma hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Rene Meza amesema kuwa tangu kuanzishwa kwake, huduma hiyo imeleta mapinduzi makubwa katika sekta ya huduma za fedha kwa njia ya mtandao kwa watumiaji wa huduma za simu za mkononi zaidi ya Milioni 27 ambao wamekuwa wamkuwa wanufaika wkaubwa bila kujali mipaka ya mtanado.

    "Huduma hii ya M pesa imekuwa na mafanikio makubwa katika kubadili maisha ya Watanzania, na sio tu katika kutuma na kupokea pesa bali imekuwa na mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa nchi yetu kutokana na kuwaweka mamilioni ya Watanzania katika mzunguko wa huduma za kifedha" alisema Meza. Meza aliongeza kuwa huduma hiyo imewezeshwa na ubunifu wa kipekee ambao muda wote imewawezesha watanzania kufurahia kutuma na kupokea pesa kupitia mitandao yote huku mawakala zaidi ya 70,000 wakiwa msaada mkubwa kwa wananchi hao kuweza kutimiza miamala yao kwa urahisi, uhakika na usalama zaidi mahala popote wakati wowote.

    "Mafanikio ambayo tumeyapata tangu kuanzishwa kwa huduma hii mwaka 2008 ni namna ambavyo tumewawezesha watanzania kutuma na kupokea pesa katika mitandao yote nchini kupitia mawakala zaidi ya elfu 70000, walioenea nchi nzima, alisema Meza na Kuongeza, "Tuko katika mazungumzo na watoa huduma wengine wa fedha kupitia njia ya mitandao kuangalia namna ambavyo tunaweza kuboresha huduma hii zaidi" Aidha, Meza aliongeza kuwa utofauti wa huduma ya M pesa na huduma nyingine ni kuwa M-pesa imewezesha kwa kiasi kikubwa kuunganisha mifumo ya malipo ya biashara mbalimbali.

    "Tuko katika ushirikiano na mabenki zaidi ya 26 nchini ambayo yameunganishwa na huduma yetu, na kuwawezesha wateja kutoa pesa au kuweka moja kwa moja kwenye akaunti zao, hii ni mbali na baihsra nyengine zaidi ya 300 ambazo zimatumia huduma ya M-pesa pamoja na idadi kubwa ya mawakala zaidi ya elfu 70000 ambao pia wanatoa huduma kwa Watanzania." Alisema.

    Mkurungezi Mtendaji huyo alisema kuwa taarifa zinaonesha kuwa utumiaji mkubwa wa huduma ya M pesa ni kuweka na kutoa Pesa katika kuendesha shughuli za maisha za kila siku hivyo Vodacom itaendelea kuwawezesha Watanzania kutuma na kupokea pesa kupitia mitandao yote nchini ili kufikia malengo ya kurahisisha huduma za kifedha kwa Watanzania wote pale wanapohitaji na popote walipo nchini.

    Meza alisema kuwa zaidi ya Shilingi Trilioni 1.5, zimekuwa zikishuhudiwa kila mwezi kupitia Miamala mbalimbali inayofanywa na wateja wa huduma ya M pesa, huku ikiwa inachangia zaidi ya asilimia 35 ya pato la taifa.

    "Sisi kama Vodacom tunajivunia kuwa sehemu ya mafanikio haya makubwa katika utoaji wa huduma za kifedha na kuongeza upatikanaji wa ajira kwa Watanzania." Alihitimisha Mkurugenzi huyo.


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.