Warembo wanaowania taji la Miss Chang'ombe wakiwa katika pozi, shindano hilo litafanyika Juni 27 katika ukumbi wa TCC Chang'ombe jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu
MKALI wa kibao cha Basi Nenda Moshi Katemi 'Mo Music' anatarajia kutumbuiza katika shindano la kanda ya Temeke, litakalofanyika Julai 27, katika ukumbi wa TCC Club Chang'ombe.
Mo Music ambae anatamba na kibao hicho atakuwa sambamba na bendi ya Ruvu Stars, mchekeshaji nyota na msanii wa muziki Mussa 'Kitale' na wasanii chipukizi Rota Komba 'Rota' na Muhidini Mahussein 'Gsenior'.
Warembo 12 wamekuwa wakiendelea na mazoezi chini ya mkufunzi ambaye alikuwa mshindi wa taji la Redd's Miss Tanzania Top Model 2013, Narietha Boniface.
Warembo hao ni pamoja na Mariam Elias, Pendo Msaky, Neema Abbas, Pauline Nkini, Clars Shayo, Lilian Loth, Catherine Alex, Patricia Pontian, Jihi Abbas na Evelyn Adrew.
Temeke imewahi kutoa warembo kadhaa miaka ya nyuma waliopata mafanikio katika mashindano hayo, mitindo na kazi nyingine hasa kupata uzoefu wa kujiamini katika njanja mbalimbali.
Miongoni mwao ni Miriam Odemba(1997) aliyepata kuiwakilisha Tanzani katika fainali za mitindo zilizofanyika Nice Ufaransa na kupata mkataba wa Elite Model Look, baadaye kufakinikiwa kutwaa nafasi ya pili ya Miss Earth World, zilizofanyika China.
Pia, Temeke ilimtoa Happines Millen Magesse(2001), na kutwaa taji la Miss Tanzania na kwa sasa anang'ara sana katika tasnia ya mitindo katika nchi za Marekani, Afrika Kusini na barani Afrika kwa ujumla. 2003 Temeke ilimtoa Miss Tanzania, Sylvia Bahame na 2006 kuwatoa Jokate Mwegelo na Irene Uwoya.
Jokate alitwaa taji la Miss Temeke mwaka huu na pia kushika nafasi ya pili Miss Tanzania na pia kushinda taji la ubalozi wa Redd's na gazeti la Citizen. Uwoya ambaye alikuwa mshindi wa pili Temeke alishika nafasi ya nne kwenye Miss Tanzania mwaka huo.
Genevieve Mpangala mwaka 2010 alitwaa taji la Miss Temeke baadaye kushinda taji la Miss Tanzania.
0 comments:
Post a Comment