June 19, 2014

  • MJUMITA YASAIDIA KUOKOA MSITU WA ANGAI WILAYANI LIWALE



    MJUMITA YASAIDIA KUOKOA MSITU WA ANGAI WILAYANI LIWALE
    Na Abdulaziz ,Lindi 
    Mtandao wa Jamii wa Usimazi wa misitu Tanzania (MJUMITA) wamekuwa wakitoa elimu ya utawala bora katikavijiji 24 vinavyozunguka msitu wa Angai kuanzia mwaka 2011 kwa ufadhili wa Limas (lindi and masasi agribusiness support) Mjumita wamekuwa wakitoa elimu hiyo katika hivyo ikiwemo Uraghabishi ,utawala bora, Usimamizi shirikishi wa misitu,Uongozi na Utawala bora huku Elimu ikitolewa kwa jamiii za vitongoji juu ya uwezeshaji na utunzaji wa misitu kwa manufaa ya jamiii zilizo katika vitongoji na Vijiji wilayani Liwale 
    Akiongea na Globu ya Jamii ,Bw Frank Munuo mwakilishi wa Mjumita wilayani humo alieleza kuwa Vijiji 3 miongoni mwa vijiji 24 vilivyo katika msitu wa Angai wilayani Liwale vitaanza uvunaji mwishoni mwa mwezi huu(June)baada ya kukamilisha michakato yote hatimaye kufikia hatua ya uvunaji 
     Vijiji hivyo ni Mtawatawa, Kitogoro na Litohu vimefikia hatua hiyo baada ya elimu iliyotolewa na ikiwa ni hatua ya kipekee kwa vijiji kuanza kufaidika na misitu ya vijiji kwani kupitia Uvunaji huo asilimia 95% ya mapato yatakuwa ni kwa ajili ya kijiji na asilimia 5% ni kwa Halmashauri ya wilaya kwa ajili ya kusaidia kutoa huduma pale watakapohitajika kufanya hivyo. 
    Aidha Frank alibainisha pia Kufikia hatua hiyo yaa ya vijiji hivyo 3 kuanza uvunaji ni hatua ya kipekee kwa wanajamii kuanza kunufaika na raslimali hizi za misitu moja kwa moja imetokana na Mafunzo kwa vijiji hivyo 24 mafunzo ambayo yamesaidia utunzaji wa Misitu pamoja na kumaliza migogoro ya Vijiji ikiwemo ya Mipaka na na Utawala Bora 
    Kwa Upande wake,Mkuu wa Wilaya ya Liwale,Ephraim Mmbaga akiongea na waandishi wa habari waliotembelea wilaya hiyo alieleza kuwa Usiri wa jamiii na kuoneana haya ndio changamoto kubwa inayoathiri maendeleo ya wilaya hiyo huku raslimali zikinufaisha wachache 
     Akiongelea mpango unaoendelezwa kwa Usimamizi wa Mjumita na Limas,Mmbaga amesema ameridhishwa na Asasi hizo kwa kusaidia kutoa elimu kwa jamiii kutunza misitu yao ili wanufaike na rasilimali hizo hulu akibainisha uelewa uliopo Vijijini baada ya kupewa mafunzo ya Utawala Bora ambapo kwa sasa vijiji vinakutana kupanga mipango shirikishi ya Maendeleo Ikiwemo kubainisha mapato na matumizi,Usawa wa kijinsia,Huduma za Jamii pamoja na kulinda Misitu baada ya kuelewa manufaa yatakayopatikana
     Mashine inayotumika kukatia magogo ambayo tayari mkoa wa Lindi imepiga Marufuku kutumika kwa mashine hiyo ambayo inachangia kwa kiasi kikubwa Uharibifu wa Misitu
     Wananchi wa kijiji cha Ngunja wilayani Liwale wakiwa katika mkutano mkuu maalum wa kijiji ambao unapokea mrejesho baada ya Mafunzo yaliyotolewa na Mjumita pamoja na Limas
    Picha na Abdulaziz,Lindi


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.