Mhe. Dr. Tedros Adhenom, wa tatu kutoka kulia akiwa na wanaridha wa Watanzania wa mbio ndefu waliotia kambi mjini Addis Ababa. Wa pili kulia ni Mhe. Naimi Aziz, Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, wa Kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Ethiopia, Mhe. Balozi Solomon. Na wengine wailiokaa ni Maafisa Waandamizi wa Wizara ya Michezo ya Ethiopia. Mhe. Dr. Tedros aliwaasa wanariadha hao na kuwataka wafanye vizuri katika mashindano ya Madola yatakayofanyika huko Scotland mwezi July 2014. Alisema ushindi wa utakuwa ni wa Tanzania, Ehiopia na Afrika kwa Ujumla. Dr. Tedros vile vile aliridhishwa na kiwango cha maandalizi kilichofikiwa baada ya kupata tathmini kutoka kwa makocha.
Baadhi ya wanariadha wa Tanzania wakimsikiliza Mhe. Dr. Tedros.
0 comments:
Post a Comment