Mwenyekiti wa umoja huo(EACO) Francis Wangusi ambaye pia ni mkurugenzi mkuu wa tume ya mawasiliano nchini Kenya
Mkurugenzi mkuu wa tume ya mawasiliano nchini Uganda Patrick Mwesigwa
Mkurugenzi wa Watumiaji wa Watoa Huduma za Mawasiliano hapa nchini Dkt.Raynold Mfungahema
Balozi Joseph Bangurambona wa Burundi akiongea juu ya mkutano huo.
Wadau zaidi ya mia moja kutoka taasisi za mamlaka ya mawasiliano Afrika Mashariki (EACO} wamekutana jijini Arusha ili kuangalia namna ya kuweza kutatua changamoto zilizopo katika sekta hiyo muhimu ya mawasiliano.
Akizungumza na waandishi wa habari mwenyekiti wa umoja huo(EACO) Francis Wangusi ambaye pia ni mkurugenzi mkuu wa tume ya mawasiliano nchini Kenya alisema kuwa mkutano huo unalenga kujadili changamoto zilizobainishwa na wadau wa sekta hiyo kuhusu vikwazo ambavyo vinakwamisha mbalimbali usambazaji wa mawasiliano kwa nchi hizo.
Wangusi alisema kuwa sekta ya mawasiliano ina vitengo mbalimbali ikiwemo posta,mawasiliano ya simu na utangazaji na mitandao ya kijamii(internet) ambayo bado inakabiliwa na changamoto nyingi zinazohitaji juhudi za wadau wa sekta hiyo ili kuwafikia watumiaji.
Aidha alibainisha kuwa huduma ya posta bado inakabiliwa na changamoto ya anuani makazi ili kuwawezesha watumiaji wanaoutumia huduma hiyo iweze kuwafikia kwa haraka kama zilivyo huduma nyingine.
Hata hivyo wangusi aliongeza kuwa changamoto nyingine kubwa ni mawasiliano ya huduma za simu katika nchi za Afrika mashariki ambapo mbali na watoa huduma kupata faida kubwa lakini pia wanawatoza watumiaji gharama kubwa hivyo kupelekea watumiaji kutoka nchi moja hadi nyingine kushindwa kumudu.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Watumiaji wa Watoa Huduma za Mawasiliano hapa nchini Dkt.Raynold Mfungahema alisema lengo ni kuangalia kuwa mawasiliano yanawafikia watumiaji na kufaidi huduma hiyo ya simu,internet,utangazaji na maswala ya posta.
(Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
0 comments:
Post a Comment