June 16, 2014

  • KUWEKA SIMU MFUKONI KUNAATHIRI MBEGU ZA KIUME?SOMA HAPA



    KUWEKA SIMU MFUKONI KUNAATHIRI MBEGU ZA KIUME?SOMA HAPA
    Uchunguzi wa utafiti kutoka chuo kikuu cha Exeter nchini Uingereza, unapendekeza kuwa idadi ya mbegu za uzazi za wanaume huathiriwa kwa kuweka simu za mkononi kwenye mifuko ya suruale
    Hata hivyo ,mwana sayansi wa maswala ya uzazi na shahawa,alisema kuwa ushahidi huo bado haukuwa na uhakika wowote hivyo basi simu yake bado inaendelea kukaa mfukoni mwake.
    Uchunguzi huo uliochapishwa katika jarida la 'Environment International' ulilaumu mnunurisho wa kielectromagnetiki kuwa chanzo kikuu.
    Lilichanganua tafiti kumi tofauti kuonyesha ubora wa shahawa ikihusisha wanaume 1,492.Hii ilijumuisha kupimwa kwa shahawa zilizowekwa wazi kwa mnunurisho wa simu za rununu, kwa maabara na udadisi wa wanaume katika cliniki za uzazi
    Kiongozi wa uchunguzi huo Dkt.Fiona Mathews aliambia BBC kuwa kutokana na uchunguzi huo,moja tu ndio ulionyesha uhusiano kati ya utumizi wa simu na kudidimia kwa ubora wa shahawa.
    "Nafikiri kwa mwanamume wa makamu hakuna haja ya kuingiwa na hofu,iwapo unajua una uwezekano wa kuwa na shida ya kizazi basi itakuwa jambo la busara kutoweka simu mfukoni ,pia kugeuza mtindo wako wa kula."


    Mbegu za uzazi za wanaume zinasemekana kuathirika kutokana na simu za mkononi
    'Uchunguzi zaidi'
    Alikubali kukosolewa na wana sayansi wengine huku akiunga mkono kuwa kuna umuhimu wa kufanya uchunguzi zaidi.
    Dkt,Mathews alimaliza kwa kusema"hili ni jambo la kusisimua lakini hatusemi kwa 

     
    uhakika kuwa kila anayebeba simu mfukoni atakuwa na shida ya kizazi."
    Dkt.Allan Pacey kutoka chuo kikuu cha Sheffield anasema kuwa wazo hilo la kudidimia kwa shahawa na kuharibu "DNA"linatokana na "radio frequency" na mnunurisho wa kielectromagnetiki zinazopatikana kwenye simu na pengine joto aidha moja kwa moja kutoka kwenye simu au mnunurisho.
    Dkt huyo anayefanya uchunguzi wa shahawa bado hajashawishika akisema ushahidi huo hauna msingi na ataendelea kuweka simu mfukoni.
    Aliambia BBC,"kumekuwa na shauku kwa mda kama kuweka rununu mfukoni kunaweza changia kudidimia kwa ubora wa shahawa na nguvu za kiume kivyovyote.
    "Kumekuwa na habari zisizokuwa na msingi lakini kwa maoni yangu uchunguzi uliofanywa hadi kufika sasa haujakuwa wa kutosha kwa sababu wachunguzi aidha hawakuhifadhi shahawa vile inavyofaa ama wamedadisi matumizi ya simu kati ya wanaume bila kuzingatia mambo mengine kama mitindo yao ya maisha.
    "Tunayohitaji ni uchunguzi kufanywa ambapo utumizi wa simu unazingatiwa vile vile tabia zinazoathiri maisha yao.
    Hadi pale tutakapo tafakari hayo,nitaendelea kuweka simu yangu katika mfuko wa mkono wa kulia wa suruale yangu!"

  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.