June 19, 2014

  • Balozi Seif Ali Iddi azindua rasmi kitabu cha Historia ya Vyombo vya Habari Zanzibar


    Balozi Seif Ali Iddi azindua rasmi kitabu cha Historia ya Vyombo vya Habari Zanzibar
     Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizindua rasmi kitabu cha Historia ya Vyombo vya Habari Zanzibar hapo katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Bweach Resort Mbweni nje kidogo ya mji wa Zanzibar. Anayemsaidia kufungua ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania { MCT } Kajubi Mukanjanga na kulia ya balozi ni Mkuu wa Mkoa Mjini Maghribi Mh. Abdulla Mwinyi.
     Balozi Seif akinyanyua kopi ya vitabu viwili vinavyoelezea Historia ya Vyombo vya Hbari Tanzania kulia yake  akishangiriwa na Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mh. Abdulla Mwinyi. Kushoto ya Balozi Seif ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania Nd. Kajubi Mukajanga na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar ambae pia ni Mjumbe wa Bodi ya Baraza la Habari { MCT } Nd. Rafii Haji Makame.
     Mtafiti Kiongozi wa Kitabu cha Historia ya vyombo vya Habari Zanzibar Bibi Maryam Hamdan akiweka saini kitabu hicho mara baada ya kuzindauliwa rasmi na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi. Kulia ya Bibi Maryam ni mshauri wa Habari katika Kamati hiyo ya utafiti Bwana Ali Rashid Salim na Kushoto yake Bibi Maryam ni Mwanasheria aliyehusika na harakati za uandishi wa Kitabu hicho Bibi Fatma Saleh Amour.
     Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiwa katika Picha ya pamoja na Kamati ya utafiti wa Kitabu cha Historia ya Habari Zanzibar pamoja na Uongozi wa Ngazi ya juu ya Baraza la Habari Tanzania { MCT } mara baada ya uzinduzi wa Kitabu hicho. Kushoto ya Balozi ni Mtafiti Kiongozi wa makusanyo ya maandishi ya kitabu hicho Bibi Maryam Hamdan na Mshauri wa Habari katika Timu hiyo Bwana Ali Rashid Salim. Kulia ya Balozi ni Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Maalim Abdulla Mwinyi na Mwanasheria katika timu hiyo Bibi Fatma Saleh Amour. Waliosimama nyuma ni Uongozi wa Juu wa Baraza la Habari Tanzania { MCT } uliosimamia harakati zote za uandishi wa kitabu hicho ukiongozwa kwa Katibu Mtendaji wa Baraza hilo  Nd. Kajubi Mukajanga wa pili kutoka kulia.

    Balozi Seif akibadilishana mawazo na Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania { MCT } Nd. Kajubi Mukajanga nje ya ukumbi wa Zanzibar Beacha Resort Mbweni mara baada ya uzinduzi wa kitabu cha Histori ya vyombo vya Habari Zanzibar. Pembeni yao ni Mwanahabari mkongwe  Tanzania na ukanda wa Afrika Mashariki Salim Said Salim. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.