June 01, 2014

  • VIJANA WAASWA KUJIEPUSHA NA NDOA KATIKA UMRI MDOGO



    VIJANA WAASWA KUJIEPUSHA NA NDOA KATIKA UMRI MDOGO
    PIX 3 (2)
    Afisa Msaidizi wa Vijana kituo cha UMATI tawi la Dar es Salaam Bi. Upendo Daud akiwaeleza vijana kuhusu mada kuu ya Tamasha ambayo ni "Athari za ndoa za utotoni" wakati wa ufunguzi wa tamasha la mwezi katika kituo hicho.

    PIX 5 (1)Mwenyekiti wa mtaa wa Wailes Bw. Abdul Kidege ambaye ndiye mgeni rasmi katika Tamasha la Jamvi la vijana kituo cha UMATI jijini Dar es Salaam akitoa hotuba yake fupi kwa vijana waliohudhuria tamasha hilo lenye lengo la kuwaeleimisha vijana juu ya athari za ndoa za utotoni.
    PIX 6 (1)PIX 7Vijana wakifuatilia kwa makini hotuba ikiyotolewa na mgeni rasmi kabla ya ufunguzi wa Tamasha la Jamvi la Vijana Kituo cha UMATI jijini Dar es Salaam.
    PIX 17Vijana toka kundi la The Africa wakionesha igizo maalum linalohusu athari ya maradhi mbalimbali yakiwemo TB na Ukimwi yanayoweza kuwakumba vijana katika maisha yao ya ujana endapo hawatakuwa makini na jinsi gani ya kujiepusha nayo.
    Na Benedict Liwenga-MAELEZO, Dar es Salaam
    NDOA nyingi za utotoni husababishwa na tabia ya baadhi ya wazazi na walezi kuwalazimisha watoto wao wa kike kuolewa katika umri mdogo kwa tamaa ya kujipatia fedha ama utajiri katika familia zao jambo ambalo linawanyima haki ya kusoma watoto wengi kwani watoto hawa wanakuwa wako katika umri chini ya miaka kumi na nane.
    Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Mtaa wa Wailesi Wilaya ya Temeke Bw. Abdul Kidege wakati wa ufunguzi wa Tamasha la Jamvi la Vijana linalofanyika kila mwisho wa mwezi katika kituo cha vijana UMATI jijini Dar es Salaam.
    Bw. Kidege amesema kuwa kuna baadhi ya wazee na vijana wenye tabia ya kuwarubuni wasichana wadogo kwa kuwapa pesa na vitu vya thamani kwa lengo la kuwashawishi kuolewa nao na pia kuna baadhi ya wazazi ambao wakati mwingine ushirikiana katika kufanikisha azma hiyo jambo ambalo ni kinyume na haki za watoto katika jamii.
    "Kuna baadhi ya wasichana wenye umri mdogo wamekuwa wakinyanyaswa kijinsia kwa kubakwa na wengine kulazimishwa na wazazi wao wenyewe kuolewa na watu wazima ambao wamewazidi umri, jambo hili halikubariki na vijana nawaasa msikubali kurubuniwa kwa pesa au vitu toka kwa watu wa namna hiyo". Alisema Bw. Kidege.
    Kwa upande wake Afisa Vijana Msaidizi Chama cha Uzazi na Malezi Bora Tanzania (UMATI) Bi. Upendo Daud amewaeleza vijana waliohudhuria tamasha hilo kuwa vijana wanapohudhuria matamasha katika kituo cha UMATI wanapata fursa kubwa ya kupata elimu bure juu ya afya ya uzazi, athari za mimba za utotoni, kupima Ukimwi, ushauri nasaha, uzazi wa mpango pamoja na uelimishaji rika jambo ambalo linawafanya vijana wengi waweze kujitambua na kujikinga.
     "Hili ni Tamasha kwaajili ya vijana linaloandaliwa kila mwisho wa mwezi na Youth Action Movement (YAM) kwa lengo la kuwaelemisha vijana juu ya mambo mbalimbali yanayohusiana na afya na mada kuu ya tamasha hili kwa leo ni Ndoa za umri mdogo  na athari zake". Alisema Bi. Upendo.
    Youth Action Movement (YAM) ni kikundi cha Vijana ambacho kilianzishwa na chama cha uzazi na malezi bora Tanzania (UMATI) kwa ufadhili wa Internationa Planned Parenthood Federation (IPPF). Chama hiki cha vijana kinapatikana katika kila tawi la UMATI nchi nzima na kwa tawi la Dar es Salaam ndiyo waandaaji wa Jamvi la vijana kila mwezi ambapo husaidia kutoa huduma bure kwa vijana kuhusu afya ya uzazi, kupima Ukimwi, ushauri nasaha, uzazi wa mpango pamoja na uelimishaji rika


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.