June 22, 2014

  • VAN GAAL SASA AMTAKA DE JONG MANCHESTER UNITED …Milan iko tayari kumuachia kwa pauni mil 6


    VAN GAAL SASA AMTAKA DE JONG MANCHESTER UNITED …Milan iko tayari kumuachia kwa pauni mil 6
    VAN GAAL SASA AMTAKA DE JONG MANCHESTER UNITED …Milan iko            tayari kumuachia kwa pauni mil 6

    KOCHA mpya wa Manchester United Louis van Gaal amemtaka mtendaji wa timu hiyo Ed Woodward kufanya juhudi za kumnasa kiungo wa zamani wa Manchester City Nigel de Jong.

    Van Gaal amedhamiria kuimarisha safu ya kiungo Old Trafford na anaona de Jong ndiye mtu sahihi kufanya kazi hiyo.

    Nyota huyo anayekipiga AC Milan, ameanza mechi zote za Holland katika michuano ya Kombe la Dunia inayoendelea nchini Brazil na kuonekana kuiteka himaya ya safu ya kiungo kwenye kikosi hicho kinachonolewa na Van Gaal.

    De Jong mwenye umri wa miaka 29 amebakiza miezi 12 kwenye mkataba wake ambapo miamba hiyo ya San Siro iko tayari kumuuza kuliko kumpoteza bure mwaka mmoja baadae.

    Inaaminika Milan itakuwa tayari kumtoa kwa pauni milioni 6.



  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.