June 23, 2014

  • MAONESHO YA BIDHAA ZA TANZANIA KATIKA UBALOZI WA TANZANIA LUSAKA, ZAMBIA (TANZANIA WEEK) 25 -31 JULAI 2014



    MAONESHO YA BIDHAA ZA TANZANIA KATIKA UBALOZI WA TANZANIA LUSAKA, ZAMBIA (TANZANIA WEEK) 25 -31 JULAI 2014
     Katika kuendelea kusherehekea Muungano wetu na pia kujiunga na wenzetu wa nchi ya Zambia ambao nao mwaka huu wanasherehekea miaka 50 tangu wapate Uhuru (25 Oktoba), Ubalozi wa Tanzania nchini Zambia unapenda kuwajulisha kuwa umeandaa maonesho ya bidhaa zinazozalishwa nchini Tanzania.

    Ubalozi wa Tanzania nchini Zambia unachukua nafasi hii kuwakaribisha rasmi Watanzania kuja kushiriki katika maonesho haya. Tuna amini ni nafasi nzuri ya kujitanganza na kuonana uso kwa uso na wadau mbalimbali ili kupanua wigo wa biashara.

    Maonesho haya ambayo yamebeba jina la "TANZANIA WEEK" yatafanyika katika viwanja vya Ofisi ya Ubalozi Lusaka, Zambia, kuanzia tarehe 25 hadi 31 Julai 2014. Mwisho wa kujisajili kushiriki ni tarehe 25 June 2014.
    Kwa maelezo zaidi na mawasiliano tumia njia zifuatazo:

         Nukushi ya Ubalozi: tanzanhighcom@zambia.co.zm
         Namba ya Simu: +260211253323/4 
         
    Maafisa wa Ubalozi;
          
    i) Bibi Justa M. Nyange - simu ya kiganjani +260-979-401-433 
          Nukushi : kitutuj@yahoo.com

        ii) Bw. Richard M. Lupembe  - simu ya kiganjani +260-965-031-754
              Nukushi : rlupembe@yahoo.com.

        iii) Bw. Mogosi S. Munatta - simu ya kiganjani +260-979-411-011
              Nukushi : munatta@yahoo.co.in.
          
       iv)  Bw. Huddy A. Kiangi …….simu ya kiganjani +260-977-934-240
             Nukushi : hkiangi@yahoo.com.


    KARIBU SANA LUSAKA, ZAMBIA



  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.