June 10, 2014

  • Watanzania Watakiwa Kuchangamka Fursa za Biashara, DITF



    Watanzania Watakiwa Kuchangamka Fursa za Biashara, DITF
    Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania, TANTRADE Bibi Jaqueline Mneney Maleko akizungumza na waandishi wa habari (hawako pichani) kuhusu Maonyesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Biashara ya Nje wa TANTRADE, Bibi. Anna Bulondo.

    Umetolewa mwito kwa Watanzania kuzichangamkia fursa mbalimbali za kibiashara, zinazoletwa na Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam,  DITF ambapo Maonyesho ya huu, yatajumuisha makampuni zaidi ya kimataifa toka nchi yatashiriki.

    Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania, TANTRADE, Bibi  Jaqueline Mneney Maleko wakati akizungumzia maandalizi ya Maonyesho ya 38  Kimataifa ya Dar es Salaam,  kwa waandishi wa Habari, ofisi za TANTRADE jijini Dar es Salaam jana.

    Bibi Maleko amesema,  lengo kuu la Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara, ni kufungua fursa za kibiashara, kama fursa za kutafuta wabia, fursa za kutafuta wawekezaji, na fursa za kuona bidhaa za viwango vya kimataifa ili  wazalishaji wa bidhaa za Tanzania kujitahidi kufikia viwango hivyo vya kimataifa badala  mtindo uliopo sasa kwa watu kujitokeza kwa wingi kuja, kununua tuu bidhaa..

    Maonyesho ya mwaka huu, yatashirikisha  waonyeshaji bidhaa zaidi ya 1,200 kati yake Wizara, Idara na Wakala za serikali zaidi ya 60, na  makampuni zaidi ya 400 ya kimataifa yamethibitisha kushiriki.

    Bibi Maleko amesema  hii ni fursa nzuri kwa Watanzania na Makampuni ya Kitanzania  kujitokeza kwa wingi na kuchangamkia fursa zinazoambatana na maonyesho ya kimataifa.

    Kauli Mbiu  ya Maonyesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam ni  ni Kuunganisha Uzalishaji wa Bidhaa na Masoko, ili kutoa fursa kwa wazalishaji wa bidhaa za Tanzania,  kupata fursa za masoko ili bidhaa hizo ziweze kukidhi vigezo vya  kimataifa hivyo kuziwezesha kuingia kwenye masoko ya  kimataifa.

    Bibi Maleko, ametoa wito kwa wafanyabiashara wa Tanzania na haswa wazalishaji bidhaa za Tanzania, ili kuweza kuingia kwenye ushindani wa masoko ya ndani nay a kimataifa, ni muhimu kwanza ukajua mahitaji ya soko, ndipo uzalishe bidhaa zitakazo kwenda sambamba na mahitaji na vigezo vya masoko.

    Ameeleza kama kawaida kutakuwa na banda maalum la Tanzania lenye bidhaa za ndani zilizikidhi viwango vya kimataifa ili kuwahamasisha  Watanzania kupenda bidhaa za ndani kwa kupenda chako, jenga chako.

    Pia maonyesho ya mwaka huu tayahusisha maonyresho ya biashara za bidhaa za ubunifu na vipaji, zikiwemo bidhaa za mavazi, sanaa za maonyesho na hata zanaa za muziki, hivyo kutakuwemo wanamuzi wataoonyesha bidhaa zao za muziki.

    Bibi  Maleko ametoa wito kwa Watanzania wasio na ajira, kuzitumia fursa za maonyesho hayo ili waweze kujiajiri. TANTRADE itafanya kazi ya kuwajengea uwezo, wakiwemo watu wenye makundi maalum kama wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, hivyo TANTRADE iko kwa ajili ya kuwashika mkono, kuwanjengea uwezo, kuwatafutia mitaji, uwezo na kuwatafutia masoko.


    Bi Maloke aliwataka washiriki wote wa maonyesho hayo kufanya maandalizi mapema na kufikia tarehe 27 ya mwezi huu, mabanda yote lazima yawe yamemalizika, ili kukidhi viwango vya kimataifa vinavyosimamia  Taasisi ya Maonyesho ya Kimataifa ya UFI.


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.