June 02, 2014

  • Kombe la Dunia 2014: Italia yamuondoa Giuseppe Rossi



    Kombe la Dunia 2014: Italia yamuondoa Giuseppe Rossi
    Mshambuliaji wa Fiorentina Giuseppe Rossi ametemwa kwenye kikosi cha Italia cha wachezaji 23 ambacho kinajiandaa na fainali za Kombe la Dunia, licha ya kupona majeruhi ya goti.Rossi, 27, alicheza dakika 71 katika mchezo wa Jumatatu uliomalizika kwa sare ya 0-0 dhidi ya Jamhuri ya Ireland, lakini hakupata nafasi ya kwenda Brazil.
    Antonio Cassano amejumuishwa baada ya kuifungia Parma magoli 12 msimu huu, wakati mshambuliaji wa AC Milan Mario Balotelli ameteuliwa kwenye kikosi cha Cesare Prandelli.
    Mabingwa hao wa Kombe la Dunia mwaka 2006 wanaanza kampeni yao dhidi ya England Juni 12 na watakutana na Costa Rica na Uruguay kwenye Kundi B.
    Kiungo wa AC Milan Riccardo Montolivo ametemwa baada ya kuvunjika mguu wake wa kushoto katika mchezo dhidi ya Jamhuri ya Ireland.
    Wengine waliotemwa ni mshambuliaji Mattia Destro, kiungo Romulo na walinzi Manuel Pasqual na Christian Maggio.
    Kikosi kamili:
    Walinda mlango: Gianluigi Buffon (Juventus), Salvatore Sirigu (Paris St Germain), Mattia Perin (Genoa).
    Walinzi: Andrea Barzagli, Leonardo Bonucci, Giorigo Chiellini (all Juventus), Gabriel Paletta (Parma), Ignazio Abate, Mattia De Sciglio (both AC Milan), Matteo Darmian (Torino).
    Viungo: Andrea Pirlo, Claudio Marchisio (both Juventus), Thiago Motta, Marco Verratti (both Paris St Germain), Daniele De Rossi (AS Roma), Antonio Candreva (Lazio), Marco Parolo (Parma), Alberto Aquilani (Fiorentina).
    Washambuliaji: Mario Balotelli (AC Milan), Antonio Cassano (Parma), Alessio Cerci (Torino), Ciro Immobile (Torino), Lorenzo Insigne (Napoli).


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.