Wakati zoezi la upigaji kura likiendelea nchi nzima wakazi wa kata ya Matongo, jimbo la Bariadi, mkoani Simiyu wameshindwa kupiga kura kwa nafasi ya udiwani kwa kile kinachodaiwa uhaba wa karatasi za kupigia kura.
 Akiongea na waandishi wa            habari Msimamizi wa uchaguzi katika jimbo hilo Abdallah Malela            amesema kukosekana kwa karatasi ndicho chanzo cha uchaguzi kwa            ngazi ya udiwani kusitishwa katika eneo hilo.
         Alisema kuwa kata hiyo ina            jumla ya wapiga kura 7500, na vituo 17 lakini karatasi ambazo            zimetoka Tume ya uchaguzi zilikuwa 3400 tu, huku zaidi ya            wapigakura 4100 wakikosa karatasi hizo za kupigia kura.
        "Baada ya kuona hali hiyo              niliwasiliana na viongozi wa tume kutoa taarifa ambao              waliamua kuhairisha zoezi kwa nafasi ya udiwani tu, mpaka              tena itakapotangazwa na tume," alsiema Malela.
         Kwa upande wa rais  na            mbunge, zoezi liliendelea kama kawaida kwa kuwa karatasi hizo            zililetwa za kutosha.
         Kwa upande wa Jimbo la             Itilima  Mkoani hapa  Msimamizi wa uchaguzi Alphonce Aloyce            alisema zoezi lilienda salama licha ya mihuri kukwama ingawa            tatizo hilo lilipatiwa ufumbuzi mapema.
        
0 comments:
Post a Comment