Mpiga picha wa runinga ya taifa nchini Burundi, pamoja            na familia yake wameuawa katika mji mkuu Bujumbura.
        Polisi mjini humo wanasema kuwa walikuwa wakijaribu            kuwaokoa maafisa wenzao wa polisi waliokuwa wametekwa nyara.
        Polisi wanasema kuwa watu kumi waliuawa katika kisa            hicho akiwemo mpiga picha huyo wa runinga Christophe            Nkeza-bahizi, mkewe na wanawe wawili pamoja na afisa mmoja wa            polisi.
        Milio ya risasi na na milipuko ya mabomu yalisikika            usiku kucha.
        Ghasia nchini Burundi, zilianza mwezi Aprili mwaka            huu, baada ya Rais Pierre Nkurunziza kutangaza angewania            muhula wa tatu wa urais.
        Katika miezi ya hivi karibuni, Burundi imekumbwa na            wimbi la mauaji ya kiholela ya wanaharakati wa upinzani na            maafisa wa usalama.
        Haijajulikana mara moja ni nani aliyewateka nyara            maafisa hao wa polisi.
        
0 comments:
Post a Comment