
Na  Walter Mguluchuma
        Waumini wa Kanisa                la Kiijili  la Kilutheli  Tanzania (KKKT)  Dayosisi ya                Ziwa Tanganyika inayounda Mikoa ya Katavi na Rukwa                imepanga kufanya ibada ya misa  Oktoba  24 badala                ya  Oktoba 25 ilikuwapa nafasi waumini wa Kanisa hilo                kushiriki uchaguzi mkuu utakao fanyika Jumapili ya oktoba                25
                Hayo yalisemwa                hapo jana na Askofu wa KKT  Dayosisi ya Ziwa Tanganyika                wakati alipokuwa akizungumza na gazeti hili kwa njia ya                simu wakati akiwa Sumbawanga Mkoa wa Rukwa
         Alisema Kanisa                limeamua  kuhamishia  ibada hiyo  siku ya juma mosi badala                ya jumapili ili kutowa nafasi kwa waumuni wa Kanisa hilo                kushiriki  kakamilifu uchaguzi mkuu wa Oktoba 25
         Kanisa  linatambua                umuhimu wa uchaguzi Mkuu ndio  maana limehamisha shughuli                zake zote ambazo zilikuwa zifanyike  jumapili ya Oktoba 25                na badala yake zitafanyika jumamosi ya oktoba 24
        Nae Katibu wa                Dayosisi hiyo  Abrahamu Kombe amesema kuwa Kanisa                limefanya jambo zuri sana kuhamishia  ibada siku hiyo ya                jumamosi badala ya jumapili
         Alisema hakuna                tena muumini wa Kanisa hilo Katika  Dayosisi ya Ziwa                Tanganyika ambae atashindwa kupiga kura kwa                kisingizio  cha kuwa   alikuwa kwenye ibada
         Mpaka saa kuna                baadhi ya Madhehebu ya Dini                mbalimbali  hapa nchini  wameishatangaza  kuhamishia  ibada                zao siku ya jumamosi ya tarehe 24 badala ya tarehe 25                oktoba kwa ajiri ya kupisha uchaguzi mkuu utakaofanyika                siku hiyo wa kuwachagua Wabunge na Madiwani na Rais
        
0 comments:
Post a Comment