Bondia wa Ufilipino, Manny Pacquiao ametangaza Jumatano hii kuwa anaweza kustaafu masumbwi mwakani baada ya pambano moja la mwisho ili kujikita kwenye siasa zaidi na pengine kuwamia nafasi ya useneta.
Pacquaio aliyeokoka, amedai kuwa amechukua ushauri kutoka kwa Mungu.
"Nadhani nipo tayari kustaafu. Nimekuwepo kwenye ndondi kwa miaka 20," alisema Pacquiao, 36 kwenye mahojiano na kituo cha runinga cha ABS-CBN. "Nilimuomba Mungu aniongoze na nafurahi kuhusu hilo."
Pacquiao alianza kucheza masumbwi ya kulipwa akiwa na miaka 57, ameshinda mapambano 57, zikiwemo knockouts 38 na ameshindwa mara sita, mara tatu kwa knockouts. Ametoka sare mara mbili.
Mwaka huu alipoteza pambano lake na Floyd Mayweather.
Pacquiao ni kiongozi wa chama chake cha siasa na anatarajia kuwania useneta kwenye uchaguzi wa mwakani nchini Ufilipino.
0 comments:
Post a Comment