Waathiriwa wa ugonjwa wa Ebola wametakiwa kutumia            mipira ya kondomu hadi kutakapokuwa na ufahamu wa kutosha            kuhusu matokeo ya utafiti yanayoonyesha kwamba virusi hivyo            husalia katika majimaji ya mbegu za kiume kwa kipindi cha hadi            miezi tisa.
        Shirika la afya duniani WHO limesema kuwa maambukizi            ya ebola kupitia tendo la ngono ni kidogo mno na kutaja maeneo            ya taifa la Sierra Leone ambayo yana idadi kubwa ya manusura            lakini hayana visa vipya vinavyojirudia.
        Lakini mkuu wa WHO Margeret Chan ameiambia BBC kwamba            kuna maswali mengi.''Hatujui iwapo wanaweza kuambukiza ama            vipi ,bado hatuna ushahidi wa kutosha''.
        ''Kiwango cha ufahamu bado kinatutia wasiwasi ,ndio            maana lazima tuchukue tahadhari ,kwa hivyo tunawashauri            manusura kujilinda kupitia mipira''.
        
0 comments:
Post a Comment