Msajili wa Vyama Vya Siasa, Jaji              Francis Mutungi akizungumza na waandishi wa habari  Jumatatu              Oktoba 12, 2015  kwenye ukumbi wa mikutano uliopo katika              ofisi hiyo jijini Dares Salaam kuhusiana na masuala ya amani              kuelekea Uchaguzi Mkuu na baada ya uchaguzi huo.
        Picha zote na Magreth              Kinabo-Maelezo.
                Msanii Mrisho Mpoto akizungumza na              waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano uliopo katika              ofisi hiyo jijini Dares Salaam kuhusiana na masuala ya amani              kuelekea Uchaguzi Mkuu na baada ya uchaguzi huo.
                Mwanamziki wa nyimbo za injili              nchini, Christina Shusho akizungumza na waandishi wa habari               kwenye ukumbi wa mikutano uliopo katika ofisi hiyo jijini              Dares Salaam kuhusiana na masuala ya amani kuelekea Uchaguzi              Mkuu na baada ya uchaguzi huo.
                Baadhi ya waandishi wa habari              wakiwa katika mkutano huo.
        ………………………………………………………………….
        Na Magreth Kinabo-maelezo
        Ofisi ya Msajili wa Vyama  Vya              Siasa imewaasa na kuwataka viongozi wote wa  vyama  vya              siasa kutoa kauli na maelekezo kwa wafuasi wao na wanachama              wa vyama vyao kutoshiriki katika aina yoyote ile ya uvunjifu              wa amani hususan katika kipindi cha kuelekea Uchaguzi Mkuu              na baada  ya uchaguzi huo.
        Hayo yamesemwa  leo na Msajili wa              Vyama Vya Siasa, Jaji Francis Mutungi wakati akizungumza na              waandishi wa habari leo kwenye ukumbi wa mikutano uliopo              katika ofisi hiyo jijini Dares Salaam.
        "Dhamana  ya nchi iko mikononi              mwenu,ushawishi wenu kuhusu amani katika kipindi hiki ndio              utakaoliokoa taifa la Tanzania ama  utaliingiza taifa katika              vurugu na mfarakano," alisema Jaji Mutungi.
        Jaji Mutungi alisema katika              kipindi cha kampeni kumekuwepo na viashiria vya uvunjifu wa              amani miongoni mwa jamii yakiwemo baadhi ya makundi ya              wanachama, wafuasi na mashabiki wa vyama siasa.
        "Makundi hayo yanadiriki kutoa              maneno ya kejeli, matusi, kuvamia, kupigana, hata kujeruhi              makundi mengine, ambayo siyo ya upande wao. Hali  iiachwe              mara moja ili kuiweka nchi yetu Tanzania  katika hali ya              amani na kuiepusha kuingia kwenye vurugu, mfarakano na              machafuko yasiyokuwa na  ulazima.
        "Dumisheni amani na kamwe               tusijiingize kwenye siasa zinazoleta mfarakano na uvunjifu              wa amani, kumbukeni  kuna maisha baada ya uchaguzi na amani              ya nchi yetu ni fahari  yetu sote,alisema  Mutungi.
        Aliongeza ni vyema Watanzania,              wakatambua kwamba utofauti wa itikadiya vyama ndio ukomavu              wa demokrasia nchini hivyo ni jambo la busara kuvumiliana na              kufanya siasa za kiustaarabu.Hivyo  kutovumiliana kwa              utofauti wetu wa itikadi za kisiasa kunaweza kulata madhara              makubwa kwa jamii itakatopelekea idadi kubwa ya Watanzania              kupata athari ikiwemo ulemavu, vifo, ukimbizi,njaa na              maradhi.  
        Aidha ofisi hiyo imetoa rai kwa              waandishi wa habari watumie kalamu zao vysema kuhubiri              amani  na kuepuka kuandika habari za uchochezi, bali              wawasaidie wananchi kupata taarifa sahihi zitakazowasaidia              kufanya maamuzi wakati wa kuchagua viongozi wao.
        Kwa upande wao mabalozi wa amani,              ambao ni Mrisho Mpoto na Christina Shusho walisema kwa              nyakati tofauti kuwa wamejitolea kuhubiri amani kupitia fani              yao  ili nchi yetu iendelee kuwa na amani.
        Akizungumzia suala hilo, Mpoto              aliwapa changamoto waandishi wa habari wajiulize kuwa wana              mchango  gani  katika nchi yao ili kuhakikisha inakuwa na              amani. Hivyo wanapoandika habari yoyote wakumbuke  kwamba              kuna watoto, yatima, walemavu na wajane, isije ikawa ni              chanzo cha kuvuruga  amani.
        Naye Shusho alisema kwamba yeye si              mfuasi wa chama chochote,bali balozi wa kuhubiri amani.
        Ofisi              hiyo imetoa kauli hiyo, kwa kuwa ndiyo yenye jukumu la              kuhakikisha ukuaji wa demokrasia unakuwepo kulingana na              sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa kikatiba.
        
0 comments:
Post a Comment