Watu watatu sasa wamethibitishwa kufariki baada ya            daraja la mda kuangukia barabara kuu ya magari mjini            Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya jumatano.
        Watu wengine 19 walijeruhiwa katika kisa hicho            ,kulingana na shirika la huduma za dharura nchini humo.
        Meya wa Johannesburg amesema kuwa iwapo uchunguzi wao            utabaini kwamba kuanguka kwa daraja hilo kunatokana na uzembe,            wale waliohusika watawajibishwa kulingana na mwandishi wa BBC            Pumza Filhani mjini humo.
        Kampuni ya ujenzi nchini Afrika Kusini Murray &            Robert imeanzisha uchunguzi wake.
        BBC.
        
0 comments:
Post a Comment